HEADER AD

HEADER AD

TAASISI YA MISA TANZANIA YASISITIZA MARIDHIANO YA KITAIFA

TAASISI ya vyombo vya habari kusini mwa Afrika (Misa Tanzania) imesisitiza maridhiano ili kuendelea kua na Tanzania bora yenye amani, mshikamano na umoja.

Wakati watanzania wakiendelea  kuwafariji watu mbalimbali wakiwemo wanahabari waliopata madhila yaliyotokana na kadhia wakati wa uchaguzi hivyo inatoa rai kwa vyama vya siasa ,taasisi za dini,vyombo vya habari ,makundi ya kijamii na wananchi kutafuta suluhu  na maridhiano ya kitaifa ili kuponya majeraha 

Akitoa taamko hili kwa niaba ya taasisi hiyo  November 7,2025 Mwenyekit wa taasisi ya vyombo vya habari kusini mwa Afrika (Misa Tanzania)  Edwin Soko amesema ipo haja ya kuimarisha misingi ya haki,uhuru na amani ya nchi 

"Ni vigumu kuamini au kuelewa matukio yaliyojiri wakati  na baada ya uchaguzi  mkuu wa tarehe 29 Octoba 2025 ni matukio yaliyowaumiza watanzania kihisia ,kiakili na kimwili ,kwani zipo familia zilizopoteza wapendwa wao ,zinazowaaguza majeruhi na zilizopoteza mali na biashara huku watanzania wakikosa haki ya kikatiba ya kupata taarifa kupitia vyombo vya habari na njia za mawasiliano ya kidijitali "amesema Soko

Ameongeza kuwa, kwa namna ya kipekee  MISA Tanzania inaungana na watanzania wote kutoa pole kwa familia zilizopoteza wapendwa wao ,wanawaombea majeruhi wote wapate nafuu na  kupona haraka.

Aidha miongoni mwa walioathirika ni baadhi ya  waandishi wa habari  hivyo wanahimiza kulindwa kwa haki ya kupata taarifa

No comments