HEADER AD

HEADER AD

ASKOFU EAGT TARIME : WASIOONA MSIJIDHARAU, NYIE NI WA THAMANI

Na Mwandishi Wetu , Nyamongo

ASKOFU wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God Tanzania (EAGT) Jimbo la Tarime , Sebastian Bwiri amewataka watu wenye ulemavu wa kutoona kutojidharau bali wajione ni wa thamani kwani mwenyezi Mungu aliwaumba na kuwaona ni wa thamani.

Akizungumza katika mkutano mkuu wa Chama cha Wasioona wilaya ya Tarime uliofanyika shule ya sekondari Ingwe, amesema ulemavu hauondoi thamani mbele za Mungu .

       Askofu wa Kanisa la EAGT Jimbo la Tarime , Sebastian Bwiri akizungumza na Wanachama wa sioona wilaya ya Tarime (TLB).

" Usijidharau ,jione wewe ni wa thamani kama Mungu anavyotuona ni wa thamani. Wahitaji hawatakosa kwenye Dunia hii ni kwasababu makusudi ili wale wengine wenye vitu awapime jinsi watakavyotoa huduma kwa wahitaji.

" Kitambu cha Kumbukumbu la Torati 15: 11 inasema ; kwa maana masikini hawatokoma katika milele; ndipo ninakuamuru na kukuambia , mfumbulie kwa kweli mkono wako,masikini wako katika nchi yako" amesema Askofu .

Amewasihi watu ambao wanaona kwamba, wanalo jukumu la kuwasaidia wahitaji wasioona " Watu wenye ulemavu ni matokeo ya uimbaji wa Mungu" amesema Askofu Sebastian.













No comments