DIWANI KATA YA MATONGO- NYAMONGO ACHANGIA MILIONI MOJA CHAMA CHA WASIOONA TARIME

>>Wadau wengine nao wamo, Askofu, EAGT Tarime, Neema Isaack Range , Mama Kasimili, Waracha , Lightness Rukindo , Sake ltd , Rajabu Mining, Fregom, Bhoke Matunda
Na Mwandishi wetu, Nyamongo
DIWANI Godfrey Kegoye wa Kata ya Matango- Nyamongo ,wilayani Tarime , ametoa msaada wa fedha Tsh. Milioni moja kwa ajili ya kukiwezesha Chama cha Wasioona (TLB) wilaya ya Tarime.
Diwani Godfrey amekabidhi fedha hizo wakati wa mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika Desemba, 19, 2025, katika ukumbi wa shule ya Sekondari Ingwe-Nyamongo.
" Bhoke ambaye ni mhasibu wa TLB amekuwa akiwasiliana na mimi na kunieleza changamoto zenu, nami nimezichukua nitaziwasilisha kwenye vikao vyetu vya halmashauri .
" Kuanzia leo nipo tayari kushirikiana nanyi . Mje muandae kikao kingine tukae pamoja tujadiliane , kwa leo nawachangia Tsh. Milioni moja keshi" amesema Diwani Godfrey.
Diwani Kata ya Matongo, Godfrey Kegoye (kushoto) akimkabidhi fedha Tsh. 1,000,000 Mwenyekiti wa chama cha Wasioona wilaya ya Tarime,Desemba,19,2015 .
Katika mkutano huo wadau wametoa misaada mbalimbali akiwemo Samwel Keraryo ambaye ni mkurugenzi mtendaji kampuni ya Sake, aliyetoa Tsh. Milioni 1.2 kwa ajili ya chakula wakati wa mkutano mkuu wa TLB.
Wengine ni Rajabu Mining Tsh. 500,000, Fregom Tsh. 100,000, Askofu Sebastian Bwiri wa kanisa la EAGT Jimbo la Tarime,Tsh. 200,000 na mchele kilo 10, Christina Mniko (Mama Kasimili) Tsh. 200,000.
Askofu Sebastian Bwiri wa kanisa la EAGT Jimbo la Tarime (kulia), akimkabidhi fedha Tsh. 200,000 Mwenyekiti wa Chama cha Wasioona wilaya ya Tarime , Museti Mwita.
Pia Neema Isaack Range (Mrs Rin ) ametoa msaada wa mchele kilo 100, mafuta ya kupikia lita 20 na sabuni za unga,Lightness Rukindo (Mama Michael ) mchele kilo 60 , Bhoke Matunda mchele kilo 10 , Frola Eliudi sukari kilo 10, Mlezi wa chama hicho cha Wasioona wilayani humo Waracha ltd.Tsh 200,000.
Wawakilishi wa kampuni ya ujenzi WARACHA LTD wakimkabidhi fedha Tsh. 200,000 Mwenyekiti wa chama cha Wasioona wilaya ya Tarime.
Kila mwanachama akakabidhiwa pesa kwa ajili ya usafiri, mchele , mafuta na sabuni , wengine sukari jambo ambalo limewafurahisha wanachama hao na kuwashukuru wadau wote ambao wamekuwa mstari wa mbele kuunga juhudi za chama cha Wasioona kwa kutatua changamoto zao pindi wanapohitaji msaada.
Mtunza hazina wa Chama cha Wasioona wilaya ya Tarime Bhoke Orindo, amewashukuru wadau wote ambao wamekuwa wakijitokeza kukiwezesha Chama hicho na kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu aendelee kuwabariki ili wasiweze kupungukiwa pale walipotoa.
Mtunza hazina wa Chama cha Wasioona wilaya ya Tarime Bhoke Orindo akitoa shukrani kwa ufadhili wa mkutano na misaada mbalimbali.
" Nina washukuru sana wadau wote ambao wamekuwa wakitushika mkono, wapo wengi , kutokana na muda siwezi kuwataja wote kwa majina. Tunawaombea sana kwa Mungu azidi kuwabariki msipungukiwe " amesema Bhoke.
Mkutano huo ulihudhuliwa pia na Afisa maendeleo ya jamii Kata ya Matongo, Neema Abel, Afisa maendeleo ya jamii Kata ya Kemambo, Mary Laizer na Afisa ustawi wa jamii Kata ya Matongo, Elias Masangora.
Afisa ustawi wa jamii Kata ya Matongo, Elias Masangora, ameupongeza uongozi wa chama hicho kwa ushirikiano na kuahidi kuwa kitengo cha ustawi wa jamii kitaendelea kuwa karibu na chama hicho huku afisa maendeleo ya jamii kata ya Kemambo, Mary Laizer akisisitiza kuendelea kuwa bega kwa bega na chama hicho.
Afisa Maendeleo ya jamii Kata ya Kemambo, Mary Laizer akizungumza.
Diwani Kata ya Matongo Godfrey Kegoye (wa sita kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na wanachama Wasioona wilaya ya Tarime mkoa wa Mara.








.jpg)







Post a Comment