HEADER AD

HEADER AD

RC KAGERA : WANANCHI MSIKUBALI MTU YEYOTE KUWAGAWA

 Na Alodia Dominick, KAGERA

MKUU wa mkoa wa Kagera, Hajjat Fatma Mwassa amewasihi wananchi mkoani humo kutokubali mtu yeyote awagawe kidini, kikabila na kijinsi huku akiwashauri kuwa walimu wa kutunza amani ya nchi.

Mwassa ameyasema hayo Desemba, 18, katika dua na sala kuombea Taifa mkoani Kagera Iliyofanyika manispaa ya Bukoba, wakati wa ufunguzi wa tamasha la ijuka omuka ambalo lililozinduliwa siku hiyo na  litahitimishwa Desemba 21, 2025.

 Mkuu wa mkoa wa Kagera Hajjat Fatma Mwassa akizumgumza katika dua na sala la kuombea taifa  katika uzinduzi wa tamasha la ijuka omuka ambalo limezinduliwa leo.

"Tusikubali mtu atugawe tukemee wote wanaoendekeza  udini, ukabila na  jinsi, tuendelee kulinda umoja wetu, nitakemea vyote hivyo kwa nguvu zangu zote" amesema Mwassa

Amewataka wananchi wa mkoa wa Kagera kuwa walimu wa amani kwani mkoa huo uliwahi kuonja uvunjifu wa amani ikiwemo vita ya Kagera mwaka 1978 hadi 1979, ajali ya MV Bukoba, tetemeko la ardhi na majanga mengine hivyo hawana sababu ya kujiingiza katika majaribu mengine wanapaswa kukesha na kuomba.

‎Amewashukuru wananchi wa mkoa huo kwa kuendelea kulinda heshima ya Kagera pamoja na Taifa kwa ujumla, hasa katika kipindi cha uchaguzi na baada ya uchaguzi, kwa kuonyesha uzalendo wa hali ya juu na kutojihusisha kwa namna yoyote katika matukio ya uvunjifu wa amani.‎

“Niwashukuru sana wana Kagera, mlionesha uzalendo wa kutosha katika kipindi chote tulichopita kama Taifa, Wana Kagera hamkushiriki katika uvunjifu wa amani kwa namna yoyote,” amesema. 

Amesema kuwa, Tamasha la Ijuka Omuka 2025 litajumuisha kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo mkoani Kagera ili kuchochea maendeleo, Bonanza la Michezo, pamoja na kuenzi utamaduni wa mkoa huo ikiwemo vyakula vya asili.‎

Akitoa nasaha na kuomba dua kiongozi wa Answar Suna mkoa wa Kagera (JASUTA) Sheikh Abdulshahid Abbas,amewasihi watanzania kupenda nchi yao  kulinda rasirimali zake, kujisahihisaha na kumrejea Mwenyezi Mungu.

    Kiongozi wa Answar-suna mkoa wa Kagera  Sheikh Abdulshahid Abbas akizungumza na wananchi.

"Viongozi wa dini tujitahidi inapotokea taharuki ni bora wanyamaze, tutii sheria bila shuruti kazi ya viongozi wa dini ni kuwasawishi na kuwanasihi viongozi wetu wa juu, kiongozi akikosea mshike mkono mpeleke pembeni mnasihi"

Askofu Ayubu Silivester ambaye ni Mwenyekiti wa Makanisa ya Kipentekoste mkoa wa Kagera (CPCT), amewaomba wasomi, wataalamu na wawekezaji kuikumbuka Kagera kama nyumbani na kuendelea kuchukua hatua za makusudi katika kuendeleza mkoa huo katika nyanja zote.‎

  Mwenyekiti wa makanisa ya kipentekoste mkoa wa Kagera Ayubu Sylivesta wakati wa sala.

Tamasha la Ijuka Omuka 2025 limeanza rasmi Desemba 18, 2025, mjini Bukoba mkoani Kagera, na linatarajiwa kuhitimishwa Jumapili, Desemba 21, 2025 na tamasha hili ni la tatu tangu kuanza kwake mwaka 2023, kauli mbiu ya tamasha hili ni wekeza Kagera irudishe katika ubora wake.

No comments