PROF. MKUMBO AKAGUA ENEO LA UWEKEZAJI SINO TAN ,AELEZWA CHANGAMOTO
Na Gustaphu Haule, Pwani
WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais ,Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo,amefanya ziara ya kutembelea na kukagua eneo la uwekezaji wa Viwanda la Sino Tan lililopo Kata ya Kwala Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Vijijini Mkoa wa Pwani.
Profesa Mkumbo katika ziara hiyo ameambatana na Waziri wa Viwanda na Biashara Judith Kapinga, Waziri wa Maji Jumaa Aweso pamoja na Naibu Waziri wa Nishati Salome Makamba,Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson Saimon.
Akizungumza na Waandishi wa habari Desemba 10/2025 Waziri Mkumbo amesema kuwa lengo la ziara hiyo ni kukagua maendeleo pamoja na shughuli za uzalishaji zinazofanywa na viwanda kupitia Sino Tan pamoja na kuona changamoto zinazowakabili.
Waziri wa Nchi,ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo wa pili kutoka Kulia akikagua kiwanda cha kuzalisha majokofu kilichopo katika eneo la uwekezaji wa Viwanda Kwala katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Vijijini.Amesema dira ya Mwaka 2050 moyo wake ni ujenzi wa Viwanda na namna nzuri ya kujenga viwanda ni kupitia kongani ya viwanda ya Sino Tan kwa maelekezo ya Rais Samia lakini mwenendo wake ni mzuri kutokana na usimamizi mzuri wa Tiseza.
Mkumbo, amesema kuwa eneo hilo lina Mitaa 34 ya viwanda iliyosajiliwa na Tiseza kwa jina la Kwala industrial Park ambapo baada ya kufika katika eneo hilo wameweza kupokea changamoto kubwa nne ikiwemo ya ukosefu wa umeme wa kutosha, ukosefu wa maji ya kutosha uhitaji wa kituo cha reli ya Mwendokasi (SGR) na vilio vya kodi.
Mkumbo amesema katika majadiliano na Mawaziri wenzake wamepata nafasi ya kuona namna ya kutatua changamoto hizo ambapo wiki mbili zijazo eneo hilo watapata ongezo la umeme huku Suluhu ya kudumu ikifanyiwa kazi ya kutoa umeme katika kituo cha Chalinze.
Baadhi ya wafanyakazi katika kiwanda cha kuzalisha maduveti na mashuka cha Sino Tan wakiendelea na shughuli zao.Kuhusu suala la maji Mkumbo amesema tayari Waziri wa Maji Jumaa Aweso ametoa maelekezo ambapo upo mradi mkubwa wa maji unaogharimu kiasi cha Sh.bilioni 25 ambao utafikisha maji katika eneo la uwekezaji wa Viwanda la Sino Tan.
Akizungumzia suala la ombi la kuwepo kwa kituo cha reli ya Mwendokasi katika eneo hilo Profesa mkumbo amesema suala la SGR tayari Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan alishalitolea maelekezo na kwamba Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge tayari analisimamia jambo hilo.
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo (katikati) akikagua mashuka na maduveti yanayotengenezwa katika moja ya kiwanda kilichopo Kwala Kibaha Vijijini.Mbali na hayo,lakini pia Waziri Mkumbo amefurahishwa kuona katika eneo la uwekezaji wa Viwanda la Sino Tan ( Kwala Industrial Park) kuna kiwanda kikubwa cha uzalishaji wa vifaa vya umeme wa jua( Solar Power) pamoja na Uwekezaji wa kiwanda cha Chuma.
Amesema kiwanda cha vifaa vya umeme wa jua ni kikubwa Afrika na cha kwanza Tanzania lakini kiwanda cha chuma ni kiwanda cha kwanza Tanzania kuzalisha chuma ambapo umuhimu wa Viwanda hivyo ni mkubwa kwakuwa vinakwenda kukuza uchumi na hata kutoa ajira kwa Watanzania .
Waziri wa Viwanda na Biashara Judith Kapinga ( Kulia) pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo wakikagua kiwanda cha kutengeneza majokofu kilichopo katika eneo la uwekezaji wa Viwanda la Kwala Kibaha Vijijini walipofanya ziara ya kutembelea Viwanda vya eneo hilo Desemba 10/2025."Mafanikio haya ndio matokeo ya maoni ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan katika uwekezaji wa Viwanda hapa nchini na ndio maana amekuwa akiweka kipaumbele cha kutengeneza mazingira rafiki kwa ajili ya wawekezaji wa viwanda," amesema Profesa Mkumbo.
Hata hivyo,Profefa Mkumbo pamoja na Wizara nyingine zinazohusiana na masuala ya uwekezaji ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano pamoja na kuhakikisha wanasaidia kutatua changamoto zote zinazowakabili wawekezaji hao.
Mwenyekiti wa eneo la uwekezaji wa Viwanda la Sino Tan( Sino Tan Kibaha Industrial Park) Janson Haung, amesema kuwa anamshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuja na mpango maalum wa uwekezaji wa Viwanda uliowawezesha kupata fursa ya uwekezaji katika eneo la Kwala.
Amesema mipango yao ni kujenga viwanda zaidi ya 200 katika eneo hilo lakini hadi sasa tayari wamejenga Viwanda 20 lakini hatahivyo changamoto yao kubwa ni umeme,maji na hata kituo cha reli ya Mwendokasi.
Mwenyekiti wa kongani ya viwanda ya Sino Tan iliyopo katika eneo la uwekezaji wa Viwanda Kwala Janson Haung akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa kikao na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais , mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo aliyefanya ziara katika eneo hilo Desemba 10/2025.Huang,amesema kwasasa wanapata umeme kwa kiwango cha megawati 50 lakini mahitaji yao ni kupata megawati 70 na kwamba ukosefu wa umeme wa kutosha kunawafanya wakati mwingine kusimama suala la uzalishaji huku maji yanayotakiwa ni lita milioni 1.5.
Hata hivyo,Huang amekishukuru kituo cha uwekazaji (TIC) kwakuwa wamekuwa wakitoa msaada mkubwa katika kufanikisha ujenzi wa Viwanda hivyo na kwamba kupitia kituo hicho muda si mrefu watakuwa na viwanda vingi katika eneo hilo lakini wanahitaji huduma zote muhimu zipatikane hapo.






Post a Comment