SSPT MARA : SERIKALI IKISHUSHA BEI YA GESI MATUMIZI YA KUNI NA MKAA YATAPUNGUA
DIMA Online, Tarime
JUKWAA la Jamii Salama (SSPT) mkoa wa Mara, limesema kuwa serikali ikishusha bei ya gesi hasa kwa mitungi midogo itasaidia kupunguza matumizi ya mkaa na kuni ambayo yamechangia uharibifu wa mazingira kwa ukataji ovyo wa miti.f
Akizungumza na DIMA Online ofisini kwake, Afisa Mawasiliano wa Taasisi hiyo ya SSP mkoa wa Mara , yenye makao yake makuu wilayani Tarime, mkoani humo, Jenipher Karol , amesema bei kubwa ya gesi imechangia wananchi kuendelea kutumia kuni na mkaa kwakuwa hawana uwezo wa kumudu gharama ya gesi.
Afisa Mawasiliano wa Taasisi ya Jukwaa la Jamii Salama ( SSPT) mkoa wa Mara , yenye makao yake makuu wilayani Tarime, mkoani humo, Jenipher Karol" Ukinunua mtungi unakuwa na gesi yake ambapo kwa mtungi ndogo wa gesi bei ni Tsh. 45,000, baada ya hapo gesi ikiisha utalazimika kuijaza kwa Tsh. 25,000. Mtu anaona gharama hiyo ni kubwa sana kuzidi gharama ya mkaa na kuni ambazo unaweza kupata kwa Tsh. 500, 1000 watoto wakala chakula.
" Serikali ipunguze gharama za kujaza gesi kwenye mitungi ya gesi, ili hata mtu wa chini aweze kumudu gharama , ikishusha bei angalau Tsh. 15,000 kwa ile mitungi midogo itakuwa nafuu Sana.
" Ikifanya hivyo wananchi wengi wataacha kutumia kuni na mkaa na mazingira yetu yatakuwa bora kwakuwa uharibifu wa miti hautakuwepo" amesema Jenipher.
Ameongeza kuwa Taasisi yao imekuwa ikitoa elimu ya matumizi ya nishati safi ya kupikia ikiwemo ya matumizi ya majiko ya gesi na mitungi ya gesi.

" Tunatoa elimu kuhakikisha tunaitengeneza Tanzania ya kijani, kuelimisha watu kutokata miti , kuepuka matumizi ya kuni ili kuepuka madhara ya macho, ugonjwa wa pumu vinavyochangiwa na moshi wa kuni.
" Tukitumia nishati safi tutakuwa tumeondokana na magonjwa hayo . Hivyo niiombe serikali ishushe bei ya gesi ili kuwezesha wananchi wa hali ya chini kumudu gharama" amesema .
Jukwaa hilo la Jamii Salama linajihusisha na masuala ya utoaji wa elimu ya ukatili wa kijinsia, kiuchumi, kingono na kisaikolojia.
Kwa mujibu wa Jenipher amesema kwamba, mwezi Agosti hadi Octoba, 2025 wametoa elimu ya ukatili wa kijinsia ,katika kata ya Kenyamanyori ambapo jukwaa hilo lilifanikiwa kuwakutanisha watendaji wa mitaa, wenyeviti wa mitaa, wachimbaji wadogowadogo wa Kibaga katika machimbo ya madini ya dhahabu .


Post a Comment