NAIBU MEYA MUSOMA ASEMA UJIO WA NAIBU WAZIRI WA KILIMO FURAHA KWA WAKULIMA
DIMA Online, Musoma
NAIBU Meya wa Manispaa ya Musoma, Haji Mtete, ameshiriki katika ziara ya uzinduzi wa vifaa vya kilimo cha umwagiliaji iliyoongozwa na Naibu Waziri wa Kilimo na Umwagiliaji,David Silinde.
Katika ziara hiyo, Haji Mtete alimshukuru Naibu Waziri kwa kutembelea Manispaa ya Musoma na kwa juhudi zake katika kuimarisha sekta ya kilimo, hususan kilimo cha umwagiliaji.
Ameeleza kuwa hatua hiyo itawawezesha wakulima kuongeza uzalishaji, kipato na usalama wa chakula.
Jumla ya vikundi nane (8) kutoka Manispaa ya Musoma vimewezeshwa kwa kupatiwa vifaa vya kisasa vya kilimo cha umwagiliaji kwa ajili ya uzalishaji wa mbogamboga na matunda, hatua inayolenga kuwainua wakulima kiuchumi na kuchochea maendeleo endelevu katika sekta ya kilimo.
Manispaa ya Musoma inaendelea kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha wakulima wanapata zana na maarifa sahihi ili kufikia malengo ya maendeleo ya kilimo na ustawi wa wananchi.

Post a Comment