HEADER AD

HEADER AD

RC KUNENGE : MKOA WA PWANI UNAENDELEA KUTEKELEZA VIPAUMBELE VYA SERIKALI


Na Gustaphu Haule, Pwani 

MKUU wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge, amesema Mkoa wa Pwani unaendelea kutekeleza vipaumbele vya Serikali kwa vitendo hususani katika eneo la uzalishaji wa ajira kwa vijana.

Kunenge amesema hatua hiyo ni sehemu ya kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan iliyejipanga kikamilifu kuhakikisha uchumi wa nchi unakua kupitia uwekezaji wa viwanda.

         Mkuu wa mkoa wa Pwani akizungumza na wafanyakazi wa Kongani ya viwanda ya Gaini iliyopo Kibaha Vijijini ikiwa ni sehemu ya ziara yake aliyoifanya Januari 05 ,2026 .

Kunenge ametoa kauli hiyo Januari 05, 2026, alipofanya ziara ya kutembelea kongani ya viwanda ya Gaini Company Limited iliyopo Kata ya Kikongo katika Halmashauri ya Kibaha Vijijini  mkoani Pwani inayotarajia kuzalisha ajira zipatazo 1,500 ifikapo Machi 2026.

Amesema kuwa uwekezaji huo unaenda kikamilifu na mkakati wa Serikali wa kukuza uchumi wa viwanda pamoja na kuongeza fursa za ajira kwa wananchi hatua inayochochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika Mkoa wa Pwani na kuchangia pato la Taifa.

       Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge akizungumza katika Kongani ya viwanda ya Gaini iliyopo katika Halmashauri ya Kibaha Vijijini alipokwenda kufanya ziara Januari 05/2026 katika Kongani hiyo.

Kunenge amesema  Mkoa wa Pwani unaendelea kushirikiana na taasisi wezeshi Tanesco,Dawasa na Tanroads ili kuhakikisha hakuna urasimu wowote katika utekelezaji wa masuala ya uwekezaji hatua inayolenga kuwepo kwa nishati ya umeme, maji pamoja na miundombinu ya barabara.

Amesema  mradi wa bomba la gesi kutoka Kinyerezi hadi Chalinze tayari umefanyiwa upembuzi yakinifu wa Sh.bilioni 2.3 chini ya Shirika la Uendelezaji wa Petroli nchini (TPDC) jambo litakaloongeza ufanisi wa upatikanaji wa nishati kwa viwanda vilivyopo  mkoa wa Pwani.

         Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge akiwa katika kiwanda cha chuma katika Kongani ya viwanda ya Gaini iliyopo Kibaha Vijijini alipotembelea Kongani hiyo Januari 05/2026.

Naye Meneja wa mradi katika kongani hiyo Bradley  Muro, amesema ujenzi wa viwanda viwili umefikia hatua za mwisho ambapo kiwanda cha chuma kimefikia asilimia 85 huku kiwanda cha cubes kimefikia asilimia 95 na kwamba uzalishaji wa viwanda hivyo utaanza Machi 2026.

Hatahivyo,Muro amesema kongani hiyo itakuwa na viwanda mbalimbali vikubwa,vya kati na vidogo ambapo vitakuwa vinahusika katika  uzalishaji wa Nondo, Mabati,bomba za chuma ,misumari na mitambo mingine.

       Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge wa pili kutoka kushoto akikagua baadhi ya viwanda vilivyojengwa katika Kongani ya Gaini iliyopo Kata ya Kikongo Kibaha Vijijini Mkoa wa Pwani.

       Ziara ya Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge katika Kongani ya viwanda ya Gaini iliyopo Kata ya Kikongo Kibaha Vijijini.


No comments