HEADER AD

HEADER AD

KESI YA MAUAJI YA RHODA YAHAIRISHWA HADI JANUARI 19, UPANDE WA MASHTAKA HAWAKUFIKA MAHAKAMANI


>>Upelelezi bado 

>>Wakili wa utetezi aomba upelelezi uharakishwe

DIMA Online, Musoma

KESI ya mauaji ya Rhoda Jonathani mwenye umri wa miaka 42 aliyeuawa kwa kukatwakatwa mapanga akiwa nyumbani kwake Kijiji cha Burunga, Kata ya uwanja wa Ndege ,wilaya ya Serengeti mkoani Mara,  imeahirishwa hadi Januari, 19,2026.

Kesi hiyo imetajwa Jumatatu Desemba 5 2026 ikiwa ni mara ya tatu kusomwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Musoma ,mbele ya Hakimu mkazi mkuu wa Mahakama hiyo, Eugenia Rujwahuka.

Kesi hiyo inawahusisha washatakiwa  Mwalimu anayefundisha shule binafsi ya msingi Mbalali, mkoani Mbeya , Marco Marco Maginga mwenye umri wa miaka 47 na Mwita Abel Maginga (45) mkulima mkazi wa wilayani Tarime, wakikabiliwa na mashtaka ya mauaji ya Rhoda Jonathan.

       Washtakiwa wa kesi ya mauaji ya Rhoda Jonathan aliyekuwa mkazi wilayani Serengeti mkoani Mara.

Hakimu mkazi mkuu wa mahakama hiyo, Eugenia Rujwahuka amesema upande wa mashtaka hawakufika mahakamani na kwamba umeeleza kuwa upelelezi bado haujakamilika hivyo kuomba kupangiwa tarehe nyingine.

"Upande wa mashtka hawapo mahakamani leo, wametoa taarifa kuomba tarehe nyingine kwa njia ya mfumo, na kwasababu hiyo tunaahirisha kwa muda wa siku 14 hivyo tarehe ya kesi hii itatajwa tena Januari 19,2026,"amesema Rujwahuka.

Wakili wa utetezi, Mluge  Fabian ameomba kuharakishwa kwa upelelezi ili kuruhusu hatua zingine kuendelea kwa maelezo kuwa wateja wake wamekaa ndani kwa muda mrefu.

"Mtuhumiwa wa kwanza alikamatwa Oktoba 29, 2025 na wa pili alikamatwa Novemba 13, 2025 na wote walifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Desemba 12, 2025 huu ni muda mrefu sana naomba upelelezi ukamilike ili tuendelee na hatua zingine,"amesema Wakili Mluge.

Kwa mara ya kwanza watuhumiwa hao walifikishwa katika  mahakama hiyo Desemba 12 ,2025 na kufunguliwa shauri lenye namba 23/12/2025 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama ya hakimu Mkazi Musoma.

Ilielezwa mahakamani hapo kuwa washtakiwa hao wanadaiwa kumuua  Rhoda kwa kumkatakata  kwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake na kusababisha kifo chake baada ya kumvania nyumbani kwake kijijini Burunga.

Ilelezwa kuwa tukio hilo lilitokea Oktoba 23,2025 majira ya saa mbili usiku  ambapo inadaiwa washtakiwa hao walifika nyumbani kwa Rhoda kwa lengo la kufanya tukio hilo.

>>Rejea  

Kwa undani zaidi rejea habari zilizoripotiwa katika chombo hiki cha habari , Desemba, 23, 2025 yenye kichwa cha habari kisemacho ' MENEJA TARURA ALIYEKUWA AMESHIKILIWA POLISI KWA TUHUMA ZA MAUAJI AACHIWA, WAWILI WAFIKISHWA MAHAKAMANI'
 
Oktoba, 26,2025 iliripotiwa habari yenye kichwa cha habari 'MKE WA MENEJA TARURA AUAWA KWA KUKATWAKATWA MAPANGA SERENGETI. Oktoba, 26,2025 ikiripotiwa habari ' WAMUOMBA RAIS SAMIA, SERIKALI YA MARA KUWASAKA NA KUWAWAJIBISHA WALIOMUUA MKE WA MENEJA TARURA'

Pia Oktoba, 27, 2025 chombo hiki cha habari kiliripoti habari ' FIDIA UJENZI WA UWANJA WA NDEGE SERENGETI HUWENDA IKAWA CHANZO CHA KUONDOA MAISHA YA MKE WA MENEJA TARURA'.

Oktoba 28,2025 ikiripotiwa habari ' MWILI WA RHODA ALIYEUAWA KWA MAPANGA WAENDELEA KUSOTA MOCHWARI, NDUGU WAGOMA KUZIKA. Novemba, 7,2025 iliripotiwa habari ' SERIKALI KUWAFIKISHA MAHAKAMANI WALIOHUSIKA MAUAJI YA MKE WA MENEJA TARURA'.

No comments