RC PWANI, WANANCHI WAPANDA MITI SHULE YA MSINGI CHUMBI
Na Gustaphu Haule, Pwani
MKUU wa mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amewaongoza Wananchi wake katika zoezi la kupanda Miti katika Shule ya Msingi Chumbi "A"iliyopo Wilayani Rufiji Mkoani Pwani.
Kunenge ameongoza zoezi hilo Januari 27/2026 ikiwa ni sehemu ya kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ambaye anafanya sherehe ya kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa.
Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya kupanda Mti katika Shule ya Msingi Chumbi iliyopo Wilayani Rufiji Januari 27.Alisema Januari 27 ni siku ya kuzaliwa kwa Rais Samia ambaye katika kusherehekea siku hiyo Rais Samia ameona apande miti katika eneo la Kizimkazi mahali ambapo alizaliwa.
Kunenge,amesema kuwa katika kumuunga mkono Rais Samia Serikali ya Mkoa wa Pwani imeamua kupanda miti katika maeneo Wilaya mbalimbali za Mkoa Pwani .
Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge akipanda mti katika Shule ya Msingi Chumbi iliyopo Wilayani Rufiji ikiwa ni sehemu ya kuwaongoza Wananchi katika kuunga mkono siku ya kumbukizi ya kuzaliwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ambaye alizaliwa Januari 27.Amesema kuwa kwa siku ya Januari 27 jumla ya miti 6,379 imepandwa ambapo kati ya hiyo Miti 671 ni ya matunda na 5,708 ni miti ya mbao na kivuli ambayo imepandwa kwenye maeneo ya shule na katika Taasisi.
Kunenge ametoa wito kwa Wananchi na viongozi mbalimbali kuhakikisha wanaitunza miti hiyo ili kuweka kumbukumbu ya Rais Samia na hata kusaidia katika uhifadhi wa mazingira.
Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Luteni Kanali Faustine Komba akipanda Mti katika Shule ya Msingi Chumbi Wilayani Rufiji ikiwa ni sehemu ya kuzaliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan Januari 27."Leo Januari 27 ni siku ambayo Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt.Samia Suluhu Hassan alizaliwa na katika kusherehekea siku hiyo Rais amepanda miti katika eneo la Kizimkazi lakini nasisi wananchi wa mkoa wa Pwani tumeona tuungane nae kwa kupanda miti katika maeneo mbalimbali.
Kunenge amewashukuru wakazi wa Wilaya ya Rufiji hususani katika Kijiji cha Chumbi kwakujitokeza kwa wingi katika hafla ya upandaji miti hiyo huku akiwaomba kujenga tabia ya kupanda miti mara kwa mara.
Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge akipanda mti Januari 27 kumuunga mkono Rais Samia siku yake ya kuzaliwa.Aidha,katika hatua nyingine Kunenge amezindua mpango wa ugawaji miche ya korosho kwa wakulima wa Mkoa wa Pwani ambapo uzinduzi huo umefanyika katika Kijiji cha Chumbi "A".
Kunenge amesema mkoa wa Pwani utagawa bure miche 1,500,000 sawa na asilimia 35.7 ya miche 4,200,000 ambayo inatarajia kutolewa kwa Wakulima wa zao la korosho nchini Tanzania.
Amesema wa ugawaji miche hiyo ni mpango wa Rais Samia katika kuhakikisha anawainua Wananchi wake kiuchumi kupitia Kilimo na kwamba yeyote atakayepata miche hiyo lazima aitunze ili kumpa heshima Rais Samia.
Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Chumbi Wilayani Rufiji akipanda mti siku ya kumbukizi ya kuzaliwa kwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan Januari 27.





Post a Comment