HEADER AD

HEADER AD

WAZIRI SANGU : PSSSF JIPANGENI UTEKELEZAJI DIRA YA MAENDELEO 2050


Na Mwandishi Wetu, Pwani

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi na Mahusiano, Deus Sangu, amezindua Baraza la Tatu la Wafanyakazi la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF).

Waziri huyo amewataka watumishi wa mfuko huo kujipanga kwa kuanza safari ya utekelezaji wa Dira ya Taifa Maendeleo ya mwaka 2050 Julai mwaka huu.

Uzinduzi huo umefanyika Januari 31, 2026 kwenye shule ya uongozi ya Mwalimu Nyerere mjini Kibaha mkoa wa Pwani.

“Jambo kubwa lililoelekezwa kwenye Dira 2050 ni kukuza uchumi na kuzalisha ajira, tuhakikishe fedha tunazowekeza ziweze kuchochea ukuaji wa uchumi na pili iwe ni miradi ambayo inaweza kuzalisha ajira kwa vijana,” amesema Sangu.

Ameipongeza PSSSF kwa kuvuka lengo la makusanyo ya michango kutoka lengo la kukusanya Tsh. Trilioni 1.1 hadi kufikia trilioni 1.2 katika kipindi cha Julai – Desemba 2025.

Amelipongeza Baraza kwa ushauri mzuri kwa Menejimenti hali ambayo imepelekea mafanikio ambayo PSSSF imeyapata.

“ Jukumu letu sisi wafanyakazi ni kuwa wazalendo, kujituma na kutanguliza maslahi ya taifa mbele,” amesitiza.

Naye Mkurugenzi mkuu wa PSSSF,  Fortunatus Magambo, amesema uwepo na kukutana kwa Baraza hilo ni utekelezaji wa takwa la kisheria ambapo, tangu PSSSF ilipoanzishwa 2018 imekuwa ikizingatia takwa la kisheheria kikamilifu.

“Ili kupanua wigo na kuleta ufanisi mahali pa kazi, baraza letu limeundwa kwa kujumuisha Menejimenti ya Mfuko, wawakilishi wa wafanyakazi kutoka kila Kanda, kutoka Kurugenzi na Vitengo na wajumbe kutoka chama cha wafanyakazi TUICO na wajumbe wa TALGU,” amefafanua.

Kuhusu masuala yaliyojadiliwa katika Baraza hilo, Magambo amesema ni taarifa ya utendaji ya nusu ya mwaka Julai-Desemba, 2025, ambapo miongoni mwa yaliyofanyika kwa mafanikio ni ukusanyaji wa michango wa trilioni 1.2 katika kipindi cha nusu mmwaka, lengo la kukusanya trilioni 1.1, huku ulipaji wa Mafao ni Bilioni 883 sawa na asilimia 99 ya kuulifikia shilingi jadiliwa ni mafanikio ya ukusanyaji michango makusanyo ya michango.










No comments