TUHESHIMU NIKABU
VAENI
kujistiri, na msivae Kwa ria,
Ninakupeni hadhari, vyema mkinikariri,
Chukueni ushauri, utumieni vizuri,
Nikabu iheshimuni ivaeni Kwa stara.
Kwa stara ivaeni, haya ni yangu maoni,
Nikabu ithaminini, maovu sifichieni,
Nyuso zenu funikeni, Kwa nikabu jipambeni,
Nikabu iheshimuni ivaeni Kwa stara.
Nikabu ni vazi zuri, tena vazi la heshima,
Si vazi lenye dosari, kalibariki karima,
Huongeza ujasiri, kiafya pia salama,
Nikabu iheshimuni ivaeni Kwa stara.
Ni vazi lenye thamani, na tena ni vazi bora,
Siyo vazi la kihuni, limethibiti ubora,
Ni kubwa yake thamani, si vazi lenye hasara,
Nikabu iheshimuni ivaeni Kwa stara.
Vishawishi huondoa, vizuri likitumika,
Nikabu huashiria, tabia njema hakika,
Sivae Kwa mazoea, muogopeni rabuka,
Nikabu iheshimuni ivaeni Kwa stara.
Ina faida hakika, vumbi huzuia pia,
Nikabu haina shaka, ni kizuizi cha jua,
Nikabu yakubalika, si vazi lenye udhia,
Nikabu tuiheshimu tuivae Kwa stara.
Imeridhia na dini, nikabu inatambua,
Huongeza na imani, Kwa wale wanaovaa,
Si leo tangu zamani, nikabu zimeenea,
Nikabu iheshimuni ivaeni Kwa stara.
Wavaaji wa nikabu, pongezi nawapatia,
Nikabu siyo adhabu, kairidhia jalia,
Na wala siyo aibu, Kwa yule aliyevaa,
Nikabu tuiheshimu tuivae Kwa stara.
Msiogope vaeni, mjikinge na shetani,
Naelekea mwishoni, ninatua kituoni,
Nikabu tuithamini, isiwe ria machoni,
Nikabu tuiheshimu tuivae Kwa stara.
Mtunzi ni SirDody Dody
Mudio Islamic Seminary.
Moshi Kilimanjaro.
Soyakijijini@gmail.com
0671159555, 0762396923,
.jpg)
Post a Comment