Home
/
A
/
BIASHARA/UCHUMI
/
BARRICK NORTH MARA YAOMBA SERIKALI KUINGILIA KATI WATU 75 WALIOGOMEA UTHAMINI, FIDIA
BARRICK NORTH MARA YAOMBA SERIKALI KUINGILIA KATI WATU 75 WALIOGOMEA UTHAMINI, FIDIA
>> Imeelezwa kuchelewa kufanyiwa uthamini, kuchukua fidia kunakwamisha shughuli za mgodi
Na Mwandishi Wetu, Nyamongo
UONGOZI wa mgodi wa dhahabu wa Barrick North Mara uliopo Nyamongo,wilaya ya Tarime mkoani Mara , umeiomba serikali kuingilia kati watu 75 ambao kati yao wamekataa kusaini mikataba, kutochukua hundi zao na wengine kugoma kufanyiwa uthamini pamoja na fidia.
Hayo yameelezwa wakati wa kikao cha Barrick North Mara kilichowakutanisha viongozi wa serikali za vijiji 11vinavyozunguka mgodi huo, ambapo Mwenyekiti wa kikao hicho alikuwa ni mkuu wa wilaya ya Tarime, Meja Edward Gowele .
Viongozi wa serikali za vijiji 11 vinavyozunguka mgodi wa Barrick North Mara wakiwa kwenye mjadala wa maendeleo baina yao na mgodi wa Barrick North Mara uliopo Nyamongo wilayani Tarime.
Kikao hicho kilizungumzia maendeleo na changamoto ndani ya vijiji hivyo 11 vinavyozunguka mgodi ikiwa ni pamoja na kupokea taarifa ya ya mgodi ya utendaji kazi ikiwemo utekelezaji wa miradi ya maendeleo kupitia fedha za uwajibukaji wa makampuni kwa jamii (CSR) , kikao kilichofanyika ukumbi wa mgodi wa Barrick North Mara Nyamongo.
Meneja mkuu Mgodi wa Barrick North Mara , Apolinary Lyambiko amesema wanakabiliwa na changamoto ya watu kugoma kufanyiwa uthamini ili kupisha maeneo kwa ajili ya shughuli za mgodi huku wengine wakigomea hundi jambo ambalo linarudisha nyuma shughuli za mgodi .
Meneja mkuu Mgodi wa Barrick North Mara , Apolinary Lyambiko akizungumza na viongozi wa serikali za vijiji 11 vinavyozunguka mgodi wa Barrick North Mara.
" Baadhi ya Wananchi wamegoma kufanyiwa uthamini ili kuachia maeneo hayo kwa shughuli za mgodi. Wengine wamegoma kuchukua Hundi zao , wamegoma kusaini mikataba" amesema Meneja mkuu Apolinary.
Meneja Mahusiano mgodi wa Barrick North Mara, Francis Uhadi amewaomba viongozi wa serikali washirikiane kwa pamoja ili watu wakubali kuchukua fidia .
Meneja Mahusiano mgodi wa Barrick North Mara, Francis Uhadi akizungumza na viongozi wa serikali za vijiji 11 vinavyozunguka mgodi wa Barrick North Mara.
Francis amesema kwamba mpaka kufikia tarehe 19, Februari 2026 , wananchi 653 kati ya 728 wamefidiwa sawa na asilimia 89.7 .
Amesema wananchi wapatao 75 kati yao walikuwa bado hawajasaini mikataba na wengine wamekataa kufanyiwa uthamini.
Amesema waguswa walipewa fursa ya kuamua aina ya fidia " waguswa 571 walichagua fidia ya fedha tasilimu , waguswa 35 walichagua ardhi na nyumba mbadala , 37 walichagua ardhi mbadala na waguswa 10 walichagua nyumba mbadala " amesema Francis .
Ameongeza kusema " Maendeleo ya ujenzi wa nyumba za waguswa 10 zimekamika, nyumba 24 zimefikia asilimia 70, nyumba 16 zimefikia asilimia 10, 18 zipo kwenye manunuzi.


.jpg)











.jpg)




.jpg)


Post a Comment