HEADER AD

HEADER AD

MKURUGENZI KIWANDA CHA KUCHAKATA TAKA BUKOBA AISHUKURU SERIKALI KWA KUTAMBUA UMUHIMU WAO

Na Alodia Dominick, Bukoba

MKURUGENZI wa kiwanda cha kuchakata  taka za plastiki pamoja na mifuko cha Waste Plastic Enterprises kilichopo Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera  Justin Nsabi ameishukuru Serikali .

Ameishukuru serikali kwa  kuwaunga mkono, kuwapa moyo na kutambua umuhimu wao wa kutunza na kuhifadhi mazingira kwa kukusanya taka na kuzibadilisha kuwa fursa ya ajira kwa wananchi wa Bukoba.

Nsabi ametoa shukrani hizo kwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Festo Dugange alipotembelea kiwanda hicho na kukagua shughuli za uhifadhi wa mazingira kiwandani.

Mkurugenzi wa kiwanda cha West Plastic Enterprises Justin Nsabi akimuonyesha mazingira ya kiwanda kinachochakata taka za plastiki  Naibu Waziri ofisi ya Makamu  wa Rais (Muungano na Mazingira Festo Dugange alipotembelea kiwandani hapo.

Nsabi amejionea akina mama na vijana zaidi ya 250 wakiendea na ukusanayaji uchambuzi na uchakataji wa taka ikiwa ni njia ya kijiingizia kipato na kutunza mazingira.

"Tunaishukuru Serikali ya Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kutuunga mkono pindi tunapohitaji msaada wa Serikali hari iliyochochea maendeleo ya kiwanda hiki ambacho kimekuwa chachu ya kuzalisha ajira kwa wanawake na vijana"

"Wanaofanya kazi katika kiwanda hiki wanatoka sehemu mbalimbali za mkoa wa Kagera ambapo hujishuguulisha na ukusanyaji wa taka na kuleta kuuzia kiwanda na wengine wakichambua na kuchakata kisha kujipatia kipato"ameeleza Nsabi.

Akisoma risala ya kiwanda kwa Naibu Waziri huyo, Mkurugenzi wa raslimali wa kiwanda hicho Mudy Jumanne amesema kiwandani hapo wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa mashine ya uzalishaji wa bidhaa za mwisho mara baada ya kuchakatwa kwa taka hizo.

          kurugenzi wa raslimali wa kiwanda Muddy Jumanne akisoma risala kwa mgeni rasmi.

Ameomba Serikali kukiwezesha kiwanda chao kupata mkopo wa masharti nafuu ili waweze  kufikia malengo yao ya kuchakata kwa ubora zaidi.

Naibu waziri Dugange  amesema, Serikali itaendelea kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji ambao wanaunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita kupitia shuguli zao za kubadili changamoto kuwa fursa kama ulivyofanya uongozi wa kiwanda hicho.


         Naibu Waziri ofisi ya Rais (Muungano na Mazingira) Festo Dugange akizungumza na wafanyakazi pamoja na viongozi katika kiwanda hicho.

"Nawapongeza kiwanda chetu cha West Plastic hivyo hawa ni wadau wetu muhimu wanaosafisha mazingira yetu,kuleta ajira na kuongeza uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla hii inaendana na sera ya Serikali ya kusafisha mazingira na ustawi wa mabadiliko ya tabia nchi hongereni kwa kazi nzuri"Naibu waziri Dugange 

Amesema uwepo wa kiwanda hicho umeleta faida zaidi ya tatu kwa wakati mmoja kwa wananchi wa  Kagera na Taifa hivyo akashauri mkoa na Manispaa kuendelea kushirikiana na uongozi wa kiwanda .

Pia kuzitambua kwa wakati changamoto walizonazo  ili ziweze kufanyiwa kazi kwa sababu ni wadau muhimu kwa Serikali.

Ameeleza  kuwa, Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dk.Samia Suluhu Hassan inaendelea kuthamini mchango unaotolewa na wawekezaji  katika Sekta binafsi hususani wanaojihusisha na Utunzaji na hifadhi wa mazingira.

Amesema Serikali itaendelea kuboresha kwasababu ndiyo nia ya Rais wetu kuona wadau wanafanya kazi zao katika hari ya kuridhisha.




No comments