RC MARA AVUTIWA KAMPUNI ZA UJENZI ZINAZOTOA AJIRA KWA WANAWAKE

>>Asema wanawake wa Mara ni wachapa kazi
Na Mwandishi Wetu, Nyamongo
MKUU wa mkoa wa Mara , Kanali Evans Mtambi amevutiwa na utendaji kazi wa wanawake mafundi ujenzi , wabeba zege huku akiyapongeza makampuni ya ujenzi yakiwemo ha Nyamongo, yanayotoa ajira kwa usawa bila ubaguzi wa jinsia.
Ameyasema hayo Februari, 27, 2026 wakati akikagua mradi wa nyumba katika Kitongoji cha Magena, Kijiji cha Kewanja -Nyamongo, zinazojengwa na Mgodi wa Barrick North Mara, kwa ajili ya wananchi waliohamishwa kwenye maeneo yao kupisha shughuli za mgodi.
Mkuu wa mkoa wa Mara ,Kanali Evans Mtambi akisalimiana na wenyeviti wa vijiji Kewanja, Mjini Kati na Nyangoto vilivyopo Nyamongo.
" Wadada wa Tarime wanajituma , kila nikitembea huko nawaambia watu kwamba wana Mara sisi tunachapa kazi . Huwa wanahisi nawatania lakini simnaonaaa!.
" Wanawake oyeee, hapa kazi tu. Hongereni sana mko vizuri . Nawapongeza sana kwa nafasi hizi kwa watu wote , mnatoa kazi kwa usawa lakini pia kale kamnyororo kathamani tunakaona " amesema RC Mtambi .
Wanawake hao wajenzi wanafanya kazi katika kampuni ya ujenzi ya RIN LTD iliyoko Nyamongo ambayo ni miongoni mwa kampuni tatu zinazojenga nyumba za wananchi katika Kitongoji cha Magena waliohamishwa na mgodi.
Wanawake mafundi ujenzi kampuni ya RIN LTD ya Nyamongo wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa mgodi na serikali .
Akizungumzia ujenzi wa nyumba hizo, Meneja mkuu wa mgodi wa Barrick North Mara , Apolinary Lyambiko amesema mradi wa ujenzi wa nyumba za baadhi ya wananchi waliohamishwa kupisha shughuli za mgodi , mradi unahusisha Ekali 59 .
" Leo tumekutana hapa kujionea maendeleo ya mradi huu wa utoaji wa ardhi kwa ajili ya upanuzi wa shimo la Nyabirama . Mradi huu unalenga kuongeza ufanisi wa uzalishaji lakini pia kuhakikisha usalama kwa kupata eneo la mita 200 la hifadhi kinga kutoka kwenye shimo." Amesema Meneja.
Apolinary amesema hadi kufikia Februari, 26, 2026 , jumla ya waguswa 654 kati ya 728 walifanyiwa uthamini sawa na asilimia 89.8, hao tayari wameshafidiwa .
Meneja mkuu wa mgodi wa Barrick North Mara , Apolinary Lyambiko , akisoma taarifa ya mradi wa ujenzi wa nyumba za wananchi zilizojengwa na mgodi wa Barrick North Mara .
" Waguswa walipewa fursa ya kuchagua aina ya fidia wanayoitaka na fidia hizo ni fedha tasilimu au kuchagua kuhamishwa na kujengewa nyumba . Wengi wao 571 wamechagua fedha tasilimu, 36 wamechagua ardhi na nyumba mbadala.
" Katika ujenzi wa nyumba mbadala nyumba 10 zimeshakamikika ,24 zimefikia asilimia 70 , 16 zipo katika hatua ya awali , na 18 zipo kwenye hatua za manunuzi . Tunaendelea na kasi ili wahusika wahamie kwenye makazi yao mapya kuruhusu mgodi kuendelea na shughuli zake kwenye eneo la Nyabirama.
Moja ya nyumba za wananchi zinazojengwa na Mgodi wa Barrick North Mara katika Kitongoji cha Magena - Nyamongo.
Changamoto
Amesema pamoja na ujenzi wa nyumba hizo bado kuna changamoto, kwani waguswa 74 hawajasaini mikataba yao ya fidia na 11 walimkataa kufanyiwa uthamini.
" Mgodi umekuwa ukiendelea na majadiliano ya ana kwa ana kwa nia njema , uwazi na kuzingatia sheria ili kufikia mwafaka wa haki kwa kila mmoja . Hili ni eneo ambalo tumetoa viwanja na kujenga nyumba za waguswa .
" Ukubwa wa eneo hili ni Ekali 32 ,idadi ya viwanja vilivyopimwa ni 110 vyenye ukubwa wa mita za mraba 450 , vipo vingine 63 ukubwa wa mita za mraba 600 vipo viwanja 32 , venye ukubwa wa mita za mraba 1200 vipo 11 .
Ameongeza kuwa jumla ya viwanja vilivyogawiwa hadi sasa ni 61 na kwamba hatua zinaendelea za kuweka miundombinu mbalimbali ikiwemo umeme, maji, barabara .
Moja ya Barabara iliyojengwa eneo la nyumba za wananchi zinazojengwa na Mgodi wa Barrick North Mara katika Kitongoji cha Magena katika Kijiji cha Kewanja -Nyamongo baada ya kufidiwa ili kupisha eneo kwa shughuli za mgodi .
zinazojengwa na mgodi waliohamishwa na
Meneja Mahusiano mgodi wa Barrick North Mara, Francis Uhadi, amesema nyumba hizo zinazojengwa kila nyumba ina sebule, vyumba vitatu vya kulala, bafu na jiko.
Meneja Mahusiano mgodi wa Barrick North Mara, Francis Uhadi, akieleza jambo kwa mkuu wa mkoa wa Mara na viongozi wengine wakati wa kutembelea mradi wa ujenzi wa nyumba za wananchi zinazojengwa na Mgodi .
Akizungumza na chombo hiki cha habari , afisa ardhi halmashauri ya wilaya ya Tarime, Philipo Marach amesema baada ya kukamilika kwa nyumba hizo wananchi watakabidhiwa hati zao za nyumba na kwamba eneo hilo halina mgogoro wowote wa ardhi.
Afisa ardhi halmashauri ya wilaya ya Tarime, Philipo Marach akiwa eneo kunakojengwa nyumba za wananchi .
" Tumepima na tumetenga maeneo kwa ajili ya huduma mbalimbali za kijamii kama vile eneo la makaburi , eneo la kujenga taasisi mbalimbali kama kituo cha afya, soko, shule.
" Waliohamishwa ni wananchi kutoka Kijiji cha Nyabichune, Matongo, Mjini Kati. Hati zimeshaandaliwa siku wakikabidhiwa nyumba watakabidhiwa na hati " amesema Philipo.
Hata hivyo, mkuu wa mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi ametoa siku 90 kwa wananchi waliogoma kuhama katika maeneo yao ili kupisha shughuli za mgodi wakiwemo wale waliogoma kusaini mikataba ya fidia kuhakikisha wamesaini na wale waliokataa kufanyiwa uthamini kuhakikisha wanafanyiwa na kuondoka ili shughuli za mgodi ziendelee .
Mkuu huyo wa mkoa amesema hayo kufuatia uongozi wa Barrick North Mara hivi karibuni uliomba serikali, kupitia mkuu wa wilaya ya Tarime, Meja Edward Gowele kuingilia kati watu 75 ambao kati yao wamekataa kusaini mikataba, kutochukua hundi zao na wengine kugoma kufanyiwa uthamini pamoja na fidia jambo ambalo linarudisha nyuma shughuli za mgodi.
Ombi hilo lilitolewa Februari, 20, 2026 na Meneja wa Mgodi huo, wakati wa kikao cha Barrick North Mara, kilichowakutanisha wadau mbalimbali wa maendeleo wakiwemo viongozi wa serikali za vijiji 11 vinavyozunguka mgodi huo.








.jpg)







.jpg)



Post a Comment