SHAIRI: TUJIPAMBE NA IBADA
TUJIPAMBE na ibada, waja nakuhusieni,
Tuitafute faida, itufae kaburini,
Tunaupoteza muda, kwa mambo ya kishetani,
Tujipambe na ibada waja nakuhusieni.
Ibada tuithamini, tunapita duniani,
Si makazi duniani, makazi ni kaburini,
Tumuepuke shetani, asitulete motoni,
Tujipambe na ibada waja nakuhusieni.
Tuswali bila kuchoka, na tutoe pia zaka,
Tutafaulu hakika, ajuaye ni Rabuka,
Pepo yake tutafika, waja tutafaidika,
Tujipambe na ibada waja nakuhusieni.
Tujenge yetu Akhera, kwa kuchuma mambo mema,
Isitufike hasara, motoni tukalalama,
Kwa mungu waliobora ni kundi la waja wema,
Tujipambe na ibada waja nakuhusieni.
Tumche Mola jamani, ujumbe ninakupeni,
Nimefikia mwishoni, ibada tuithamini,
Tuwekeze kaburini, tunapita duniani,
Tujipambe na ibada waja nakuhusieni.
Mtunzi Sir Dody Dody
Mudio islamic seminary
Moshi, Kilimanjaro
0671159555

Post a Comment