HEADER AD

HEADER AD

PSSSF YATOA MILIONI 361.5 KUKARABATI CHUMBA CHA UPASUAJI HOSPITALI YA OCEAN ROAD


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MKURUGENZI Mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI), Dkt. Diwani Msemo, amesema msaada uliotolewa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) wa zaidi ya Sh. Milioni 361.5 kukarabati chumba cha upasuaji na uwekaji vifaa tiba utaleta furaha kwa wananchi.

Ameyasema hayo wakati akipokea msaada huo uliokabidhiwa na Meneja Uhusiano na Elimu kwa Wanachama (PSSSF), Bw. Omega Ngole, kwaniaba ya Mkurugenzi Mkuu Bw. Fortunatus Magambo, katika hafla iliyofanyika kwenye taasisi hiyo jijini Dar es Salaam, Februari 23, 2026.

       Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI), Dkt. Diwani Msemo, akizungumza wakati wa hafla ya kupokea msaada wa fedha zaidi ya Sh. Milioni 361.5 kutoka PSSSF kwa ajili ya ukarabati chumba cha upasuaji na ununuzi wa vifaa tiba februari 23, 2026.

“ Mlichofanya leo hii kimekuja kuleta majibu ya miaka 30 iliyopita, chumba hiki cha upasuaji kilitakiwa kuwepo tangu mwaka 1996, tunashukuru kwa kuungana na serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kupeleka furaha kwa wananchi,” alisema Dkt. Msemo. 

Amesema, msaada huo unagusa moja kwa moja maisha ya wananchi kwa kuwa na chumba cha kisasa cha upasuaji kwa wagonjwa wa saratani lakini pia vifaa vyake.

“ Tunaimani kwamba tutakuwa tumewekeza kwa watanzania lakini pia na wastaafu wetu kwasababu watahitaji hizi huduma.” Alisisitiza Dkt. Msemo.

Meneja Uhusiano na Elimu kwa Wanachama, Bw. Omega Ngole, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu, alisema, uamuzi wa kutoa kiasi hicho cha fedha ulitokana na ziara ya awali iliyobaini kuwa taasisi hiyo haina chumba cha upasuaji kinachojitegemea kwa ajili ya wagonjwa wa saratani.

       Meneja Uhusiano na Elimu kwa Wanachama, Bw. Omega Ngole, kwaniaba ya Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bw. Fortunatus Magambo, akizunguzma kwenye hafla ya kukabidhi msaada wa fedha zaidi ya Sh. Milioni 361.5 kwa ajili ya ukarabati wa chumba cha upasuaji na uwekaji vifaa tiba kwenye  Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI),  Februari 23, 2026.

Akifafanua kuhusu msaada huo, Ngole aesema, Tsh. Milioni 197,027,956 zitatumika kukarabati chumba cha upasuaji wa saratani na Sh. Milioni 164,491,270 zitatumika kununulia vifaa tiba kwa ajili ya chumba hicho.

" PSSSF inajisikia faraja kuunga mkono jitihada za serikali katika hospitali hii na sekta ya afya kwa ujumla, Mfuko unahudumia wananchi na ni vizuri pia kutowasahau wananchi ambao wengine ni wanachama wetu.” Alisema na kuongeza, msaada huo kupitia sera ya PSSSF ya uwekezaji kwa jamii maarufu kama CSI chini ya kaulimbiu ya #PSSSF Karibuna Jamii, watanzania wengi  wakiwemo wanachama wa PSSSF watafaidika.










No comments