HEADER AD

HEADER AD

SHAIRI : KARIBUNI MUDIO


NAANZA na shukrani, kwa Mungu mwenye dunia, 

Aliyeumba majini, pamoya na watu pia, 

Ni muweza Rahmani, yote kisha kadiria, 

Tumhimidi Jalia angali bado wazima. 


Baada ya shukrani, kwenye mada narejea, 

Napenda kuwajuzeni, wazazi wadau pia, 

Mudio fika shuleni, elimu wanaitoa, 

Sekondari ya mudio ni kisima cha Elimu. 


Ina walimu mahiri, tena waliobobea, 

Wanafundisha vizuri, kwa vitabu kurejea, 

Kwa kufundisha hodari, kila mbinu hutumia, 

Sekondari ya mudio ni kisima cha Elimu. 


Elimu mbili hutoa, ya mazingira na dini, 

Vigezo huzingatia, kwa elimu kuthamini, 

Watu wengi imetoa, wengine ni marubani, 

Sekondari ya mudio ni kisima cha Elimu. 


Watoto wenu leteni, wapate elimu bora, 

Watasoma darasani, hawatapata hasara, 

Watakuwa washindani, watatamba kwa ubora, 

Sekondari ya mudio ni kisima cha Elimu. 


Maktaba yake nzuri, vitabu imeshehini, 

Inatumika vizuri, watoto huithamini, 

Inayo mengi mazuri, nayasema si utani, 

Sekondari ya mudio ni kisima cha Elimu. 


Tumeshinda mitihani, ya kitaifa na ndani, 

Shule haiko shakani, shule yetu ni shindani, 

Kaibariki manani, ni shule yenye thamani, 

Sekondari ya mudio ni kisima cha Elimu. 


Namaliza mudio panavutia, 

Mwakaribishwa hakika, mazuri kushuhudia, 

Siyo shule ya mashaka,  ubora yajivunia, 

Sekondari ya mudio ni kisima cha Elimu. 

Mtunzi Sir Dody Dody

Mudio islamic seminary

Moshi, Kilimanjaro

0671159555

No comments