Home
/
HABARI KITAIFA
/
WAANDISHI WA HABARI, WAMILIKI WA MAUDHUI MTANDAONI TARIME WAIPONGEZA SERIKALI KUPUNGUZA GHARAMA ZA ADA YA LESENI
WAANDISHI WA HABARI, WAMILIKI WA MAUDHUI MTANDAONI TARIME WAIPONGEZA SERIKALI KUPUNGUZA GHARAMA ZA ADA YA LESENI
Na Mwandishi Wetu, Tarime
WAANDISHI wa Habari wilayani Tarime, mkoa wa Mara ,wameipongeza serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, kwa kushusha ada ya leseni kwa watoa huduma ya maudhui mtandaoni kutoka Tsh. 500,000 hadi Tsh. 50,00 tu.
Pia ada ya maombi ya leseni kutoka Tsh. 50,000 hadi Tsh. 10,000, Online Content Aggregators ( Wadau wanaokusanya maudhui) ada imepunguzwa kutoka Tsh. 1,000,000 hadi Tsh. 100,000.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma anayejulikana kama Mwana FA akizungumza kwenye mkutano wa watoa huduma za utangazaji uliofanyika Februari, 12, 2026 Dodoma , amesema mageuzi hayo yanalenga kurahisisha upatikanaji wa leseni kwa watoa maudhui mtandaoni.
Wakizungumza na DIMA Online , Waandishi wa habari na wamiliki wa vyombo vya habari vya mtandaoni wilayani Tarime mkoani Mara, wamesema hatua hiyo imeleta furaha kwa watoa maudhui .
Mwenyekiti wa umoja wa kuwezesha waandishi wa habari na wapiga picha wilaya Tarime , Jacob Karoli ameipongeza serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kupunguza ada ya leseni.
" Naipongeza serikali inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan lakini pia natoa pongezi Kwa wizara ya habari, Sanaa michezo na utamaduni inayoongozwa na Paul Christian Makonda , pamoja na Naibu waziri Hamis Mwinjuma aka. Mwana FA, kwa kazi nzuri ambayo wamekuwa wakifanya katika wizara hiyo .
" Tunashukuru serikali kwa kitendo cha kusikiliza kero na changamoto iliyokuwa ikiwatesa wanahabari pamoja na wamiliki wa vyombo vya habari za mitandaoni .
" Kitendo cha serikali kupunguza ada ya lesseni kutoka shilingi laki tano hadi elfu Hamsini kiukweli kitasaidia wamiliki wa online Television katika utendaji kazi na kuongeza ufanisi mkubwa.
" Shilingi Laki tano ilikuwa kero kubwa sana ,mtu kulipia laki tano kila mwaka ukilinganisha na hali ya kiuchumi inakuwa ngumu kwake ,hivyo wengi walikata tamaa ya kuendelea kuendesha mitandao yao kutokana na gharama kubwa .
Jacob ameongeza kusema " Kwa sasa tunaamini hakuna mtu atashindwa kulipia shilingi elfu hamsini. Kiukweli naipongeza serikali kwa hatua hii imewakomboa wanahabari kwa kiwango kikubwa .
" Mwenyekiti huyo wa umoja wa kuwezesha waandishi wa habari na wapiga picha wilaya Tarime, ametoa wito kwa wanahabari wenzake kuchangamkia fursa hiyo ili vyombo vya habari viwe vingi.
" Hii itarahisisha wananchi kupata habari kwa wakati kutokana na kuwepo kwa ongezeko la vyombo vya habari vya mitandaoni , na hii itaongeza ajira kwa vijana walio wengi hasa wale waliosomea uandishi wa habari badala ya kutegemea kuajiriwa sasa wataweza kujiajiri kupitia vyombo vya habari vya mitandaoni kama vile , Television, Blogu n.k.
" Naipongeza sana serikali kwa hatua hii maana imeleta mageuzi makubwa katika uwanja wa Tasnia ya habari Nchini, lakini pia imepanua wigo mpana kwa wananchi kupata habari.
Mwandishi wa habari wa Jambo TV Helena Magabe, amesema kuwa serikali imefanya jambo jema kushusha gharama za ada hata kwa mtu mwenye uwezo wa chini wa kifedha ataweza kumudu gharama za usajili.
" Serikali imenifurahisha sana kwa kupunguza gharama kutoka 500000 hadi 50,000 ,tunashukuru sana . Kwasababu si vyombo vyote vya online vinaingiza fedha ama vina matangazo .
" Kuna vyombo vya habari vipo kwa ajili ya kuhabarisha , kuelimisha si vya kutangaza matangazo kuviingizia fedha . Kuna waandishi walitamani kuwa na online zao lakini walishindwa kuanzisha kutokana na ada kubwa ya leseni ila sasa kwa punguzo hilo wataweza kumudu kuanzisha" amesema Helena.
Helena amemshukuru Waziri wa Wizara hiyo, Paul Makonda kwa kutekeleza ahadi aliyoahidi kwa serikali kutoa Ruzuku ya Bilioni mbili kuwezesha waendeshaji wa maudhui mtandaoni jambo ambalo tayari utekelezaji wake umeanza ambapo waombaji wameshajisajili kuomba ruzuku hiyo .
" Tunaomba fedha hizo ziwafikie walengwa kusiwepo kujuana juana , ama kupendelea vyombo vyenye majina makubwa . Nivema macho yakamulikwa kwa online zilizopo pembezoni hususani zilizopo wilayani kuliko kujikita vyombo vilivyopo mjini tu " amesema .
Mwandishi wa habari wa Gazeti la Nipashe , Timothy Itembe amesema kuwa mbali na punguzo hilo la ada serikali itilie mkazo waanzilishi wa maudhui mtandaoni kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya uandishi wa habari .
" Online zitumike kwa kufuata maadili na kwa weledi, zisiingiliwe na wajanjawajanja . Mtu akianzisha Blog iwanufaishe wananchi na serikali ipate mapato yake na sio kujinufaisha mtu mmoja " amesema Itembe.
Mmiliki wa DIMA ONLINE Blog , Dinna Maningo, ameipongeza serikali " Kiukweli serikali imejua kunikuna kabisa , ile laki tano iliumiza online nyingi na hata kuwafanya wengine kushindwa kulipa ada na kuendesha online bila usajili,matokeo yake kuwa na online nyingi zisizo na usajili kwasababu walikosa uwezo wa kifedha kusajili.
" Kama ni kweli na siyo siasa serikali itakuwa imezinusuru media nyingi za online zilizokuwa zimeshindwa kijiendesha kutokana na ada kubwa, lakini pia waliokuwa wanakwepa kusajili watasajiriwa online zao . Pia wale waliokuwa na nia ya kuanzisha online lakini wakashindwa kwasababu ya ada kubwa sasa wataweza kulipa ada na kuanzisha online.
Ameongeza " Punguzo hilo litaiwezesha serikali kupata mapato mengi maana watakaosajiliwa watakuwa wengi ikilinganishwa na wale waliokuwa wakimudu laki tano ambao walikuwa ni wachache na hivyo kundi kubwa kukwepa kulipia leseni . Punguzo hilo litawagusa watanzania wengi wenye nia ya kuendesha maudhui mtandaoni " amesema Dinna .






Post a Comment