ZAKA MEDIA STUDIO YATWAA TUZO YA MPIGA PICHA BORA KANDA YA ZIWA
STUDIO ya Zaka Media iliyopo wilayani Tarime Mkoani Mara, imeibuka mshindi wa tuzo ya mdau Shupavu kipengere cha Mpiga picha bora (Photographer) Kanda ya Ziwa.
Tuzo hizo zimezotolewa usiku wa kuamkia Jana Jijini Mwanza katika ukumbi wa Gold Crest hotel zilozoandaliwa na Kampuni ya Hollysmile.
Mkurugenzi mtendaji wa Zaka Media Fredrizzo Samsoni.Kampuni hiyo imeandaa mashindano ya mdau Shupavu mwaka 2026 yanayoendelea katika mikoa ya Kanda ya Ziwa ambapo Zaka Media Studio imekuwa mmoja kati ya washindi zaidi ya 50 wa tuzo mbalimbali zilizotolewa.
Zaka Media Studio imeibuka mshindi wa tuzo hizo ikiwashinda, Lio Bland, Junior Montana, na Jay Millions Hd.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo, Mkurugenzi mtendaji wa Zaka Media Fredrizzo mbali na kuwashukuru waandaaji wa tuzo hizo, ameishukuru familia ya Zaka Media Studio na Wateja wake na wadau ambao wamefanikisha Ushindi wa tuzo hizo kwa kuwapigia kura.
Mkurugenzi mtendaji wa Zaka Media Fredrizzo Samson.




Post a Comment