MAONESHO YA MIFUGO KANDA YA ZIWA 2026 KUFANYIKA SHINYANGA

MAONESHO ya Mifugo Kanda ya Ziwa (Lakezone Livestock Expo) yanatarajia kufanyika Mei 30-31 mwaka huu, Busanda Mkoani Shinyanga, ambapo wadau mbalimbali wa mifugo wanatarajiwa, kushiriki.
Kwa mujibu wa Diana Lukio Ambaye ni Mwandaaji wa maonesho hayo, amesema kwamba maonesho yatawakutanisha wafugaji, wakulima na wadau wote kwenye mnyororo wa thamani kutoka Mikoa ya Shinyanga, Mara, Simiyu, Mwanza, Geita, Tabora na Kagera.
"Ni maonesho ya kihisitoria ambayo yatakuwa na vitu vingi vya kujifunza juu ya ufugaji wa kisasa, masoko, fedha, bima za mifugo, breeds and feeds za kisasa.
" Karibu tujifunze na kuwekeza kwenye ufugaji biashara". Kwa wanaotaka kushiriki ama udhamini wanaweza kuwasiliana moja kwa moja na waandaji kwa namba +255762918153 .
Ameongeza kuwa hadi sasa hatua za awali zinaendelea za maonesho hayo na kauli mbiu ni " Ufugaji Biashara"
Pia yataambatana na mabanda mbalimbali ya wadau, huku kukiwa na shughuli za minada, maonesho, biashara ya bidhaa mbalimbali za mifugo na wadau na Ngoma za Asili.
Post a Comment