OMUKAMA RUHANGA AZIOMBEA NCHI ZA AFRIKA ZISIKUMBWE NA MACHAFUKO YA KIVITA
Na Alodia Babara, Uganda
Omukama Ruhanga Owobusobozi Bisaka ameziombea amani nchi za Afrika ikiwemo nchi ya Uganda kutokana na machafuko yanayoendelea katika nchi za Kiarabu yasisababishe athari katika nchi za Afrika.
Akiwa katika Makongamano yalilofanyika Mwezi Machi 2026 huko Kihihi Nyandama wilaya ya Isingiro na Wilaya ya Kyenjojo nchini Uganda, mamia ya watu kutoka ndani na nje ya Afrika Mashariki walikusanyika kuombewa, kupata baraka na mafundisho kuhusu imani ya umoja (The faith of Unity).
Omukama Bisaka anasema, watu wanapaswa kuendelea kuziombea amani nchi za Afrika na kuwa na umoja kwani kufanya hivyo watakuwa na maendeleo.
Omukamu Ruhanga Owobusobozi Bisaka akizungumza na wafuasi wa imani ya The faith of Unity katika makongamano yaliyofanyika wilaya ya Isingiro pamoja na wilaya ya Kyenjojo nchini Uganda.
Omukama Ruhanga Owobusobozi Bisaka anapokuwa na makongamano maeneo mbalimbali nchini humo, chini ya ulinzi mkali kutoka Majeshi ya Ulinzi na Usalama ya Serikali ya Uganda, hupokelewa kwa maadamano na maelfu ya watu.
Viongozi katika imani hiyo, Omukama Ruhanga Owobusobozi Bisaka, Abhakwenda (wakuu wa Dayosisi) na Abhaheleza( Watumishi) huvalia kanzu nyeupe bila viatu miguuni.
Omukama Bisaka hutoa mafundisho kwa wafuasi wake, kuwekea mikono wagonjwa na wahitaji wenye changamoto za kimaisha na wote wanaoamini huku wakitaja shida walizonazo na watu hao hushuhudia kupokea miujiza ya uponyaji kutoka kwake.
Katika makongamano hayo wagonjwa walioletwa kwa kubebwa huondoka katika madhabahu yake wakitembea wenyewe wakielezea kupona huku wengine wakileta zawadi za vitu na fedha kama shukrani baada ya kuondokana na matatizo mbalimbali na kufanikiwa katika maisha yao baada ya kuombewa.
Imani ya Umoja (Faith of Unity) haiamini katika Biblia pamoja na Madhehebu na dini nyingine zilizotokea nchi za Magharibi pamoja na zile imani za jadi.
Imani hiyo uhimiza waumini wake kuhifadhi tamaduni nzuri za Kiafrika zinazoleta watu pamoja na kuwafanya waishi kwa amani na upendo katika familia na jamii kwa ujumla. Huimiza watu kuchukia umaskini kwa kufanya kazi kwa bidii, wanawake na wanaume kupendana na kuheshimiana katika ndoa pamoja na ukalimu kwa wageni.
Omukama Bisaka anazidi kujizolea umaarufu ndani na nje ya Bara la Afrika kutokana na mafundisho yake ya kuhamasisha watu kuwa wamoja, uadilifu, amani na upendo pamoja na kuwa watu wema wakitumia salaam yao ya Umoja ya '' Okwahukana Kuhoileho'' Maana yake Kutengana Kumeisha)
Imani ya The Faith of Unity badala ya Biblia hutumia maandiko katika kitabu chake chenye mafundisho kilichosainiwa na Mwasisi wa imani hiyo na kuchapishwa na chuo kikuu cha Makerere nchini Uganda mwaka 1987.
Wafuasi wa imani hiyo hutumia kitabu hicho kuapa katika Mahakama za Uganda, hutumika kufundisha elimu ya imani katika vyuo vikuu nchini Uganda lakini pia hutambuliwa na Bunge la nchi hiyo.
"Kazi ya Mungu ni kufundisha siyo kusimulia au kuhadithia hapa siyo dini bali ni sehemu ya uponyaji mimi nafundisha umoja na watu ninaowafundisha matendo yao yanafananafanana"
"Kwa watu hawa hakuna muumini wa dhehebu lolote mfano Mkatoliki, Mlutheri, Msabato wala Muislamu bali wote ni wamoja ingawa wametoka katika madhehebu hayo" anasema Omukama Bisaka.
Anaeleza kuwa, mwaka 1980 ndipo miujiza ilianza kutendeka baada ya Omukama Ruhanga Owobusobozi Bisaka kumponya mama mmoja ambaye baada ya kuwekewa mikono alianza kuwasaidia mama waliobeba ujauzito wa mapacha kujifungua salama wakati awali walikuwa wakifariki wakijifungua.
Zipo shuhuda za watu wakielezea namna imani ya The Faith of Unity ilivyosaidia kupunguza imani za kishirikina hasa eneo la Bunyoro nchini Uganda.
Omuheleza Tweheyo Rutabajuka kutoka taasisi ya chakula duniani (WFP) Kyangwali Wilaya ya Kikuube nchini Uganda anasema kuwa, baada ya kumpata Omukama Ruhanga Owobusobozi Bisaka amewaletea amani katika maisha yao.
Rutabajuka anawaita waafrika kujiunga na Omukama Bisaka ambaye alikuja kama binadamu anakula, anakunywa analala kama binadamu wampende, wamsikilize maana anajua machungu na uzuri wa watu waje awafundishe wajue neno la Mungu.
Naye Siperansia Nestory kutoka Wilaya ya Kyerwa nchini Tanzania anasema, alijiunga na imani ya The faith of unity miaka zaidi ya mitatu sasa na alikuwa na mtoto wa kike wa miaka tisa aliyekuwa akitoroka nyumbani na kulala popote lakini tangu alipowekewa mikono na Omukama Ruhanga Owobusobozi Bisaka amepona hatoroki tena nyumbani.
Anasema, mtu yeyote anapokuwa na matatizo mbalimbali Omukama Bisaka anamwombea na kumuwekea mikono anapokubali mafundisho yake akawa mwadilifu, mwaminifu, mwenye upendo, umoja na mshikamano anabarikiwa.
"Huyu ni Mungu maana chochote unachomuomba anakubariki unakipata hatumii ushirikina wala dawa za kienyenji anapenda mila na desturi za Afrika
maombi na kuwawekea watu mikono, nilimuomba akamponya mtoto wangu" anasema Nestory
Akitoa ushuhuda namna alivyotendewa muujiza na Omukama Bisaka Omuheleza (mtumishi) Bahati John kutoka wilaya ya Kyerwa nchini Tanzania anasema kuwa tarehe 19 Februali 2021, mtoto wake wa miaka mitatu alitoweka katika Mazingira ya kutatanisha.
Anafafanua kwamba, kitongoji kizima Cha Rushwa katika kijiji cha Businde walikusanyika na kutafuta bila mafanikio na kuwa tukio hilo lilimlazimu kuomba msaada kwa shemeji yake ambaye kipindi hicho alikuwa Omuhereza katika Imani ya The Faith of Unity ili afanye maombi kwa Mungu Omukama Ruhanga Owobusobozi Bisaka akasaidie kupatikana kwa mwanae.
"Kwa kuwa mimi sikuwa muumini wa imani hii nilimpigia simu shemeji yangu Shukuru Sweatbert aliyekuwa akiishi eneo la Bugango wilaya ya Misenyi hapa Tanzania nikamuomba anisaidie kuwasiliana na watu wanaoweza kumfikia Omukama Ruhanga Owobusobozi Bisaka na kumweleza shida yangu"
"Mimi kipindi hicho sikuwa Omwichiliza (Muumini) lakini nilikuwa nikisikia kuwa nchini Uganda yuko Mungu mwenye uwezo wa kufanya miujiza na, baada ya Omukama Bisaka kupokea taarifa yangu shemeji yangu Shukuru alinipigia na kunielekeza sala ya kusali ya Omukama Bisaka" anasema John
Anaeleza, wakati wananchi waliendelea kutafuta huku wakiita jina la Omukama Ruhanga Owobusobozi Bisaka lwa sauti na kipindi hicho kulikuwa na mvua nyingi, watu hao waliporudi nyuma walikotoka walimkuta mtoto akiwa mzima na eneo alipokuwa mvua haikunyesha.
John anasema, tangu Omukama Bisaka alipomtendea muujiza wa kupatikana kwa mtoto wake aliyekuwa amepotea amekuwa muumini na sasa amekuwa Muheleza katika imani ya The faith of Unity anawakaribisha waafrika wote kuja kumuona Mungu nchini Uganda na kushuhudia miujiza yake.
Hata hivyo, akiwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya kuzaliwa kwa Omukama Ruhanga Owobusobozi Bisaka Mwezi Juni, 2025 Rais Yowel Kaguta Museveni wa Uganda alieleza kufurahishwa na mchango wa mafundisho ya imani hiyo kwani yamechangia pakubwa amani nchini humo.
Waumini wa imani ya The Faith of Unity wakiwa katika maandamano wakimpokea Omukama Ruhanga Owobusobozi Bisaka katika wilaya ya Kyenkojo nchini Uganda.





~2.jpg)
Post a Comment