MAREKANI NA IRAN ZAKUBALINA KUSITISHA MAPIGANO KWA WIKI MBILI
RAIS wa Marekani Donald Trump amesema nchi yake haitoishambulia tena Iran baada ya Tehran kukubali kuufungua mlango wa bahari wa Hormuz.
Trump amesema nchi yake inasitisha mashambulio dhidi ya madaraja na vituo vya umeme vya Iran, baada ya Marekani na Iran kukubali kusitisha mapigano kwa wiki mbili.
Iran kwa upande wake itafuungua mlango wa bahari Hormuz kwa kipindi cha wiki mbili iwapo Marekani haitoendelea kuishambulia.
Baraza Kuu la Usalama la Kitaifa la Iran limesema limekubali kusitishwa kwa mapigano na kwamba litafanya mazungumzo na Marekani mjini Islamabad Pakistan kuanzia Ijumaa.
Israel pia imekubali kusitisha mapigano nchini Iran lakini sio nchini Lebanon.
Chanzo : RFI

Post a Comment