HEADER AD

HEADER AD

MKURUGENZI KAMPUNI YA RADIANT AFRIKA ASEMA KIPIMO CHA MTU SIO CHEO AU PESA


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MKURUGENZI wa Radiant Africa Limited, Murtaza Adamjee, amese kipimo cha mtu sio cheo au pesa, bali uwezo wa kufikiri, kudhibiti hisia na kujijenga.

Ameyasema hayo April 18, 2026 Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Don Bosco Oysterbay,alipokuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya miaka 20 ya siku ya Matendo mema (Good Deeds Day). nchini.


Tukio hilo limewakutanisha vijana zaidi ya 700 na taasisi 40 kwa ajili ya Elimu, burudani, na kujifunza namna ya kubadili matendo mema kuwa mifumo endelevu.

"Uwezo wa kufikiri, kudhibiti hisia, na kujijenga ndio unaojenga mustakabali. Si wengi wanaotenda mema, inahitaji ujasiri, muhimu ni kujenga uwezo," amesema Murtaza.

Ameongeza kuwa, uwezo wa msingi huanza utotoni na huwajenga vijana kuendelea kuchangia jamii bila kukata tamaa.

Kiongozi wa Good Deeds Day Tanzania, Bi. Doroth Namuhisa, amesema mwaka huu harakati zinaongozwa na kauli mbiu ' Tuungane pamoja katika kufanya matendo mema kutoka moyoni '. Lengo ni kuhimiza watu kutenda mema kwa hiari, kwa kutumia muda, ujuzi na maarifa waliyonavyo.

"Tunasisitiza fikiri wema. Ukifikiria mema, utazungumza mema na hatimaye utatenda mema. Dunia inaweza kuwa salama zaidi endapo kila mmoja atachukua jukumu," amesema Doroth.

Good Deeds Day huadhimishwa kila Aprili na inachangia malengo ya maendeleo endelevu ya umoja wa Mataifa (SDGs) kupitia uhifadhi wa mazingira, afya, elimu, usawa wa kijinsia na kupunguza umasikini.

Baadhi ya wadau na taasisi na mashrika ya Serikali na yasiyo ya Kiserikali yaliyoshiriki ni pamoja:UTT AMIS, Dar City promotions,Coca Cola.

Wengine ni Natalia Foundation, Rotaract, Mega We Care, PGN Career Solutions, Young life Tanzania, Mental Health Africa, Builders of Future, ⁠Sana Mare.

Pia One Health Society, Ingu group, Jenga Wellness Hub,  ⁠Fahari Tuamke Maendeleo, Afya Connect Digital Doctors, Lupus Tanzania Organisation, ⁠Youth Voice Organization na wengineo.













No comments