REU YAKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA TAASISI ZA FEDHA WILAYANI TARIME

>>Miongoni mwa Taasisi hizo ni Benk ya CRDB, NMB , NBC .
>> Lengo kujenga mahusiano na Taasisi hizo
Na Mwandishi Wetu, Tarime
MWENYEKITI wa umoja wa kuwezesha Waandishi wa Habari na wapiga Picha Wilaya Tarime , ( Tarime Reporters Empowerment Union REU) Jacob Karoli ambaye ni Mwandishi wa Habari wa Clouds Media Mkoani Mara ,ametembelea Taasisi za fedha wilayani Tarime .
Mwenyekiti huyo amefanya mazungumzo na Meneja wa Benki ya CRDB , NMB, na NBC, lengo likiwa ni kuutambulisha umoja huo.
"Mbali na kuutambulisha umoja lakini pia kuzungumza namna ya kuujenga umoja huo wa REU katika upatikanaji wa fursa mbalimbali zinazotolewa na Taasisi hizo za fedha pamoja na kuimarisha mahusiano baina ya wanahabari na Taasisi za fedha. amesema Karoli.
Akiwa Benki ya CRDB , Meneja wa Benki hiyo Samora Juma , amemhakikishia Mwenyekiti wa REU ushirikiano wa kutosha ikiwa ni pamoja na mafunzo ya masuala ya fedha pamoja na fursa kwa wanahabari na wapiga Picha wilayani humo.
Kushoto ni Meneja wa Benk ya CRDB Samora Juma, akiwa na Mwenyekiti wa Umoja wa kuwezesha waandishi wa habari na wapiga picha wilayani Tarime.Naye Meneja wa Benki ya NBC , Noel Muhando ameihakikishia REU ushirikiano katika suala la utoaji elimu kwa wanahabari kuhusu shughuli za Benki hiyo.
Kushoto ni Meneja wa Benk ya NBC Noel Muhando, akiwa na Mwenyekiti wa Umoja wa kuwezesha waandishi wa habari na wapiga picha wilayani Tarime.Akizungumza na Meneja wa Benki ya NMB James Adam Mkoba, Mwenyekiti huyo ameiomba Benki hiyo kuendelea kushirikiana na wanahabari kama mabalozi wakubwa wa Taasisi hiyo ya fedha.
Kushoto ni Meneja wa Benk ya NMB James Adam akiwa na Mwenyekiti wa Umoja wa kuwezesha waandishi wa habari na wapiga picha wilayani Tarime.
Meneja wa NMB ameahidi kushirikiana vyema na waandishi wa Habari katika shughuli mbalimbali za Benki hiyo pamoja na kutoa mafunzo kwa wanahabari kuhusiana na masuala ya kifedha.
Mwenyekiti Karoli amewashukuru viongozi hao wa Benk kwa mapokezi mazuri na ahadi zao za ushirikiano na wanahabari .



Post a Comment