HEADER AD

HEADER AD

NIDA YAWATAHADHALISHA WANANCHI DHIDI YA MATAPELI WA MITANDAONI WAKIWADANGANYA KURASIMISHA LAINI ZAO ZA SIMU

Na Alodia Babara, Bukoba

AFISA habari wa Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA) makao makuu Alphani Mlacha amesema wananchi wapuuze jumbe ambazo zimekuwa zikitumwa na wezi wa mitandaoni wakiwadanganya kulasimisha laini zao.

Mlacha ameyasema hayo Mei 26,2026 katika maonyesho ya elimu ya juu kupitia bodi ya mikopo (HESLB) yanayoendelea katika viwanja vya soko kuu mjini Bukoba.


       Afisa habari Mamlaka ya vitambulisho vya NIDA makao makuu Alphani Mlacha akiwa kwenye banda la maonyesho akiendelea kutoa elimu kwa wananchi.

Amesema kuna watu wanaojihusisha na utapeli wa kutumia simu za mkononi ambao wamekuwa wakituma jumbe za kawaida wakidai wao ni Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA) na kuwa jumbe hizo zipuuzwe.

Mlacha ameeleza kuwa, jumbe hizo zinazotumwa kupitia simu za mkononi za watu binafsi zinapaswa zipuuzwe, kama kuna mtu ana jambo lolote kuhusu vitambuliaho vya taifa (NIDA) awasiliane na kituo chao cha huduma kwa wateja kupitia namba 0232210500.

“Ukiona watu wanadukua kitu fulani au huduma fulani ujue huduma hiyo ni ya muhimu sana kwa jamii kwahiyo NIDA ni sehemu ya muhimu kwa wananchi  wasidanganyike na watu wenye nia ovu.

" Pia mtu akikwazika kwa taarifa yoyote ambayo inahitaji maelekezo kuhusu NIDA mnashauriwa kufika ofisi za NIDA ili mpate maelekezo na kama mko mbali na mji tumia namba yetu ya mtoa huduma” amesema Mlacha.

Wakati huo huo ametaja lengo la wao kuwepo katika maonesho hayo kuwa, wanafunzi wanaotarajia kujiunga na elimu ya juu wanapata elimu kwao jinsi ya kujisajiri na kujiandikisha kwa maana ya kwamba wanapaswa kuwa na taarifa sahihi kama vile, cheti cha kuzaliwa kifanane na taarifa zao za NIDA pamoja na taarisa za wazazi.

          Vitambulisho vya NIDA ambavyo havijachukuliwa na wenye navyo.

Maonyesho hayo ya elimu ya juu yatafanyika kwa siku tano kuanzia Mei 26 hadi Mei 30, mwaka huu lengo likiwa ni kutoa elimu kwa vijana waweze kuepukana na utapeli ambao umekuwa ukifanywa na baadhi ya watu ambao si waaminifu na hujifanya maafisa wa Serikali wakati ni matapeli.

No comments