HEADER AD

HEADER AD

AFISA USTAWI WA JAMII TARIME DC AWAHIMIZA WAANDISHI WA HABARI KUELIMISHA JAMII MADHARA YA UKATILI WA KIJINSIA


>> Alishukuru Shirika la C. SEMA kwa kuwafunda Waandishi wa habari

Na Mwandishi Wetu, Tarime 

AFISA Ustawi wa Jamii halmashauri ya wilaya ya Tarime mkoani Mara , Siwema Silvester,  amewahimiza Waandishi wa habari  kutoa elimu ya vitendo vya ukatili, sababu na madhara yake kwani kwa kufanya hivyo itasaidia jamii kuelimika na kuachana na vitendo vya ukatili .

Pia amewasisitiza Waandishi wa habari kuandika habari za watu wenye mahitaji maalum zikiwemo changamoto wanazozipitia ili ziweze kutafutiwa ufumbuzi na kupata haki zao zinazostahili.

           Afisa Ustawi wa Jamii halmashauri ya wilaya ya Tarime mkoani Mara , Siwema Silvester akizungumza.

Ameyasema hayo Juni, 30/2026 wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari juu ya kuandika habari zitakazosaidia kuleta mabadiliko katika jamii ili kuachana na vitendo vya ukatili.

Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Blue Sky mjini Tarime, yaliyotolewa na Shirika lisilo la kiserikali la kutoa elimu ya kupinga vitendo vya ukatili (C.SEMA) .

         Waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo mjini Tarime.

" Wito wangu kwa Waandishi wa habari tuwe kichocheo kikubwa cha kusaidia, kujenga uelewa kwa jamii. Wananchi wajue ukatili ni nini, sababu zake na madhara yake.

" Tutoe elimu wananchi wajue ulemavu ni nini , changamoto wanazozipitia . Watu wajue Serikali kwa kushirikiana na mashirika wanasaidia vipi katika kutambua na kuthamini  haki za watu wenye ulemavu bila kuwashau Wazee.

Amelishukuru Shirika la C. SEMA kwa kutambua mchango wa Waandishi wa habari kwani kupitia waandishi wa habari wananchi wanapata taarifa mbalimbali na elimu .

" Nina imani mafunzo haya, yapo mambo mengi ambayo mmejifunza mmeshea uzoefu. Tumieni mafunzo yao kutoa elimu kwa jamii ili kusaidia kukomesha vitendo vya ukatili.

Mwezeshaji wa Shirika la C.SEMA Jene Haule ,amesema mafunzo hayo hutolewa mara kwa mara. Lengo ni kuwakumbusha waandishi wa habari kutimiza wajibu wao na kuandika habari zinazolinda heshima na utu wa watu wanaofanyiwa vitendo vya ukatili.


      wezeshaji wa Shirika la C.SEMA Jene Haule.






















No comments