MGANGA MKUU PWANI AMEIASA JAMII KUIMARISHA AMANI NA UPENDO NDANI YA FAMILIA
Na Gustaphu Haule, Pwani
MGANGA Mkuu wa Mkoa wa Pwani Kusirye Ukio, ameiasa jamii kuimarisha amani na upendo ndani ya familia ili kuepusha migogoro inayosababisha kuongezeka kwa idadi ya watoto wanaoishi na kufanya kazi Mitaani .
Dkt. Ukio ametoa kauli hiyo Juni 29/2026 wakati akizindua mradi wa Watoto waishio na kufanya kazi Mitaani hafla ambayo ilifanyika katika Manispaa ya Kibaha kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo Maafisa Ustawi wa Jamii , Viongozi wa dini, na Wakuu wa Dawati la Jinsia kutoka Jeshi la Polisi.
Mganga Mkuu wa mkoa wa Pwani Kusirye Ukio akizungumza katika uzinduzi wa mradi wa watoto wanaoishi na kufanyakazi Mitaani hafla iliyofanyika Juni 29/2026 .
Amesema kuwa mradi huo wa miaka mitatu ambao unatekelezwa na serikali kwa kushirikiana na Shirika la SOS Children's Village unalenga kuwasaidia watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani kupata mazingira bora ya kuishi kama ambavyo watoto wengine wanaishi.
Aidha Dkt. Ukio amesema migogoro ya kifamilia, ikiwemo kutengana kwa wazazi, ukatili wa majumbani na ukosefu wa malezi bora, ni miongoni mwa sababu zinazosababisha baadhi ya watoto kukimbia makazi yao na kuishia mitaani hali inayowaweka katika hatari ya kukumbwa na vitendo vya unyanyasaji na ukatili wa kijinsia,matumizi ya dawa za kulevya na uhalifu.
Amesema kuwa jukumu la malezi na ulinzi wa mtoto linapaswa kutekelezwa kwa ushirikiano kati ya wazazi, walezi, viongozi wa dini ,jamii na taasisi mbalimbali ili kuhakikisha watoto wanakulia katika mazingira salama na yenye kuwajengea maadili mema.

Baadhi ya maafisa Ustawi wa Jamii wakishiriki uzinduzi wa mradi wa watoto wanaoishi na kufanyakazi Mitaani,hafla iliyofanyika Juni 29/2026 katika Manispaa ya Kibaha.
Amesema mradi huo unatarajiwa kusaidia na kuboresha maisha ya watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani kupitia huduma za ushauri nasaha, elimu, afya, pamoja na kuwaunganisha tena na familia zao pale inapowezekana.
Aidha amelishukuru shirika la SOS kwa kufika katika Mkoa wa Pwani na kuahidi kutoa ushirikiano ili kusaidia kuokoa watoto waishio na kufanya kazi mitaani.
Mratibu wa mradi huo kutoka Shirika la SOS Children's Village Damas Damas amesema lengo la mradi huo ni kupunguza idadi ya watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani na kuhakikisha wanapata fursa ya maisha bora na mustakabali wenye matumaini.
Mratibu wa Shirika la SOS Children's Village Damas Damas katika uzinduzi wa mradi wa watoto uliofanyika Juni 29/2026 katika Manispaa ya Kibaha.
Amesema kazi kubwa wanayoifanya ni kupunguza wimbi la watoto wanaoishi mitaani kwa kuhakikisha wanawachukua na kuwapeleka katika vituo vya kulelea watoto na wale ambao wanataka kurudi kwa Wazazi wao uwarudisha lakini kwa uangalizi maalum.
Baadhi ya maafisa Ustawi wa Jamii wakiwa katika picha ya pamoja na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kusirye Ukio mara baada ya uzinduzi wa mradi wa watoto wanaoishi na kufanyakazi Mitaani uliofanyika Juni 29/2026 Kibaha Pwani.
Amesema watoto ambao watarudishwa kwa Wazazi wao au walezi watawekewa mtu maalum ili kuhakikisha wanapata huduma zote muhimu ikiwemo chakula ,malazi na mavazi na kwamba hata wale watakaopelekwa katika vituo vya watoto watakuwa wanafuatiliwa kwa karibu zaidi ili kujua maendeleo yao.
Hatahivyo,Damas amesema kwa upande wa Mkoa wa Pwani mradi huo unatekelezwa katika Halmashuri tano ambayo ni Mkuranga, Bagamoyo, Chalinze, Kibaha vijijini na Manispaa ya Kibaha.

Post a Comment