HEADER AD

HEADER AD

MSEMAJI WA SIMBA AHIMIZA MASHINDANO YA MWIJAGE CUP KUWA ENDELEVU

Na Alodia Dominick,  Muleba

‎MSEMAJI wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally, amemtaka mwandaaji wa Mashindano ya Mwijage Cup ambayo yanahusisha timu 20 za ndondo kutoka katika Tarafa ya Kamachumu Wilayani Muleba mkoani Kagera, kuyafanya kwa malengo ya muda mrefu na yenye kuibua vipaji kuliko kusubiri muda wa kuomba kura au jambo fulani linalohusu maslahi  binafsi.

Ally ametoa rai hiyo June 07,2026 wakati akizindua mashindano hayo katika uwanja wa mpira wa polisi Kamachumu ulioko katika kata ya Kamachumu.

       Ahmed Ally akikagua timu za Bafanabafana na Ruhanga katika uzinduzi wa ligi hiyo.

Mashindano hayo yanalenga kuwasaidia vijana kujengewa uwezo wa kucheza mpira wenye viwango vya kimataifa, kuinua vipaji na kutengeneza vipaji vipya kwenye mpira wa miguu kutoka ngazi za chini  watakaokwenda kucheza kwenye timu kubwa hapo baadaye.

"Jamii mnapaswa kumuunga mkono mwanzilishi na mdhamibu wa mashindano haya (Paul Mwijage) ili aendeelee kuwafanyia mema wana michezo hasa wakazi wa Tarafa Kamachumu.

"Malengo ya mdhamini ni kuwaunganisha nyinyi hususani vijana kupitia michezo, hivyo yawe endelevu na siyo kama wafanyavyo baadhi ya watu mfano wakati wa uchaguzi watu wanaanzisha ligi alafu wasipofanikiwa ndo inakuwa mwisho wa mashindano hayo"amesema Ally.

Msemaji wa Simba amesema amefurahi kufika Kamachumu na kukutana wanachama wa Simba na wapenda michezo, "nimeona kuna mwamko mkubwa wa michezo hasa mpira wa miguu, tumuunge mkono Mwanzilishi wa mashindano haya ambaye amewafanya vijana kuonekana kupitia vipaji vyao vya mpira" amesema.

Pia amesisitiza kualika watu wenye maamuzi katika ligi hiyo wakati ikiendelea ili wafanye usajili wa vijana kutoka maeneo mbalimbali pia kushirikisha wataalamu ambao wamesomea mpira ili waweze kupata wachezaji kutoka ngazi ya chini.

                  Wechezaji

"Haya mashindano siyo ya kubeza yanaibua vipaji ambavyo sisi tulioko huku juu hatuwezi kuvigundua mfano sisi Simba tuliwahi kupata mchezaji mzuri aitwaye Seleman Mwalimu kutoka kwenye timu ndogo ya Hai kule mkoani Kilimanjaro hivyo,huku chini kuna vipaji"amesema.

Paul Mwijage ambaye ni mdhamini na muandaaji wa mashindano hayo amesema, lengo la mashindano hayo ni kukuza vipaji vya vijana ambao wanateketea kwa ulevi, madawa ya kulevya,yatima wasio na msaada hivyo kupitia mashindano ya mpira wa miguu wataweza kuyatumia kama fursa kujiunua katika masuala mbalimbali kwa kutumia vipaji vyao.

       Paul Mwijage mdhamini na mwandaaji wa ligi akizungumza katika uzinduzi wa ligi hiyo.

‎"Lengo la mimi kuja kuwekeza nyumbani kwa kuanzisha ligi hii ni kutaka kukuza vipaji vya michezo kwa vijana wengi wanaopoteza matumaini katika soka, tumelenga Kusaidia kukuza soka la Tarafa Kamachumu,Wilaya ya Muleba,Mkoa  na Taifa.

" Ndiyo maana tumemleta Msemaji wa Simba  Ahmed Ally ili na yeye aone kuwa hata vijijini kuna vipaji vya mpira kutoka kwa Vijana wetu" amesema Mwijage.

Mwijage ameeleza kuwa, timu 20 kutoka tarafa ya Kamachumu zitashiriki katika ligi hiyo ambayo itaendelea kwa kipindi cha miaka 10 huku akiwashauri vijana wenzake kurudi kuwekeza nyumbani.

Naye Afisa michezo na utamaduni wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba Denis Joseph amesema wao kama Serikali ni yao ni kuwaunga mkono wale wote wenye nia ya kuanzisha ligi kama hizo waje waibue vipaji na wasikate tamaa lengo ni kuibua na kupata wachezaji wazuri ambao ni alama ya kuitangaza Wilaya hiyo ndani na nje ya nchi.




Mashabiki

No comments