NINI MAANA YA KIZINGITI CHA MLANGO...
NAANZA na shukrani, kwa Allah mwenye dunia,
Aliyeumba majini, pamoja na watu pia,
Ni mjuzi mwenye shani, yote amekadiria,
Kizingiti cha mlango maana yake ni nini.?
Washairi nijuzeni, majibu nipatieni,
Nami nataka baini, maana yake ni nini,?
Si leo tangu zamani, neno hili siyo geni,
Kizingiti cha mlango maana yake ni nini.?
Ukifika mlangoni, utakiona kwa ndani,
Ukifunga kuliani, chafunguka kushotoni,
Chanishangaza jamani, kina nipa mtihani,
Kizingiti cha mlango maana yake ni nini ?
Watungi jitokezeni, wa bara na visiwani,
Kwa pamoja unganeni, majibu nipatieni,
Msidhani niutani, nauliza kwa yakini,
Kizingiti cha mlango maana yake ni nini.?
Kalamu naweka chini, bandari nimefika,
Mashaka niondoeni, nitafurahi hakika,
Kwenye giza nitoeni, sitaki kuhangaika,
Kizingiti cha mlango maana yake ni nini.?
Mtungi
SirDody Dody
Mudio Islamic seminary
0671159555.

Post a Comment