HEADER AD

HEADER AD

WASHAIRI FANYENI NASI KAZI DIMA ONLINE


MKO wapi washairi, dima inawasubiri,

Hebu kateni shauri, twayangoja mashairi,

Dima itayahariri, yatasomeka vizuri,

Yatumeni mashairi dima inayasubiri.


Lengo la dima jamani, vipaji kuendeleza,

Dima inawathamini, watunzi tunawajuza,

Tungo zenu zitumeni, dima itazisambaza,

Yatumeni mashairi dima inayasubiri.


Na dima kazi fanyeni, mengi mtajipatia,

Mtakuwa washindani, tungo zenu kupitia,

Zitakuwa zenu fani, nchi itawatambua,

Yatumeni mashairi dima  inayasubiri.


Hata tenzi andikeni, jamii burudisheni,

Vipawa vyenu kuzeni, dima tawasaidia,

Na kwa beti shindaneni, ni mbali mtafikia,

Yatumeni mashairi dima inayasubiri.


Tungo zinaelimisha, jamii hufurahia,

Tena zinaburudisha, pia zinasisimua,

Hakika zafurahisha, kwa mafumbo kutegua,

Yatumeni mashairi dima inayasubiri.


Kiswahili kinakua, kwa watungi kupitia,

Sasa tunajivunia,  kiswahili meenea,

Na kwa kasi kimekua, kinazidi kusambaa,

Yatumeni mashairi dima tunayasubiri.


Nahitimisha safari, watunzi twawaalika,

Nafupisha tahariri, bandarini nimefika,

Nimesema kwa uzuri, tungo zinahitajika.

Yatumieni mashairi DIMA inayasubiri.


Mtungi.

SirDody Dody.

Mudio Islamic seminary.

0671159555

No comments