HEADER AD

HEADER AD

PROF. MKENDA AKABIDHI VITABU VYA KIDATO CHA SITA VYA ELIMU YA DINI YA KIISLAMU BAKWATA, AIPA KONGOLE TET


Mwandishi Wetu,  Dar es Salaam

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Tkenolojia, Mhe, Prof. Adolf Mkenda amekabidhi Vitabu vya Dini ya Kiislamu (EDK) kidato cha Sita kwa Baraza Kuu la Waisalam wa Tanzania (BAKWATA), Ofisi ya Mufti Mkuu Zanzibar huku akipongeza Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) kwa kufanikisha Vitabu hivyo.

Waziri Prof. Mkenda amekabidhi Vitabu hivyo 22/7/2026  katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Mfalme Muhhamed wa Sita (Bakwata Makao makuu), na kuudhuriwa na wadau mbalimbali wa dini ya Kiislamu, wakiwemo viongozi wa dini na Serikali.

Awali, Mhe. Waziri Prof. Mkenda amesema: Serikali itaendelea kutekeleza Sera ya Elimu katika kuhakikisha kila mwanafunzi nchini anapata elimu iliyo sawa  na yenye ubora.

       Waziri wa Elimu, Sayansi na Tkenolojia, Prof. Adolf Mkenda akikabidhi Vitabu vya Dini ya Kiislamu (EDK) kidato cha Sita kwa Baraza Kuu la Waisalam wa Tanzania (BAKWATA).

Ameishukuru BAKWATA kwa kuweza kusaidia mchakato wa kuwezesha Vitabu hivyo kwani kupitia Mufti Mkuu, waliweza pia kuanzisha mpango wa taasisi ya kusimamia ufundishaji wa dini ya Kiislamu shuleni (TISTA).

"Mchakato huu umefanywa kwa karibu sana na Waisalam wote, kama tulivyopata Baraka ya Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, lakini pia Mufti Mkuu na wadau wote wa dini ya Kiislamu.

"Kupitia TISTA chini ya BWAKATA hakuna Mwanafunzi atakayekosa elimu yenye ubora. Kila mwanafunzi nchini atapata elimu kwa ubora kama wanafunzi wengine  na leo hii tumekabidhi vitabu vya elimu ya dini kwa wanafunzi wa kidato cha sita nina imani kuwa vitatumika sawa sawa na ilivyokusudiwa" amesema.

Katika maboresho ya Sera ya Elimu na Mitaala yaliyofanyika mwaka 2023, maoni mbali mbali ya kuanzishwa kwa somo  la elimu ya dini ya Kiisilamu yalitolewa na wadau na baadae kuwezeshwa kwa mchakato wa uandishi wa vitabu hivyo vilivyokabidhiwa kwa TISTA kupitia Baraza la Waisilamu nchini (BWAKWATA). 

 Prof. Mkenda, ameishukuru TET kupitia Mkurugenzi  Mkuu, Dkt.Aneth Komba kwa kuhakikisha kuwa uandishi na uchapaji wa vitabu  wa vitabu unamalizika kwa haraka jambo ambalo litasaidia wanafunzi kuanza kuvitumia shueleni.

Mwenyekiti wa TISTA, Bw.Musa Kundecha ameshukuru kwa upatikanaji wa vitabu  amabvyo ameeleza kuwa ni hatua nzuri katika ufundishaji na ujifunzaji wa somo  la dini ya Kiisilamu.

Naye mwakilishi wa Mufti Mkuu wa Tanzania, Naibu Kadhi, Bw. Ali Ngeruko amesema kuwa ni hatua muhimu katika elimu ya wanafunzi katika  dini nakuwa  italeta chachu ya kuendelea kujifunza zaidi huku akiishukuru Serikali kwa jitahada  za uletaji wa vitabu kama ilivyoahidi.

Vitabu hivyo vitagawiwa katika shule zote Tanzania Bara na Visiwani ambapo wanafunzi wanaosoma somo hilo wataweza kufikiwa.






No comments