HEADER AD

HEADER AD

MRADI WA BOMBA LA MAFUTA ULIOTAKIWA KUKAMILIKA MWEZI ULIOPITA WAKWAMA


Na Alodia Dominick, Muleba

Mradi wa bomba la mafuta uliotarajia kukamilika mwezi Julai mwaka huu 

umekwama kuanza kutokana na vipuli vinavyotoka nje ya nchi kutofika kwa wakati.

Vipuli hivyo ambavyo havikutajwa vinatoka nchi gani vimekwamisha kuanza kusukumwa kwa mafuta ambayo yalitarajiwa kuanza kusukumwa mwezi Julai mwaka huu badala yake mradi huo utaanza rasmi Februari mwaka kesho baada ya kukamilika kwake.

Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Derick Moshi, aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa TPDC, amesema kuwa, mradi wa bomba la mafuta ulitarajia kumalizika rasmi mwezi Julai mwaka huu lakini kutokana na vipuli ambavyo vinapaswa kutoka nje ya nchi vimekwamisha mradi.

       Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Derick Moshi akizungumza na waandishi wa habari katika Kituo kilichopo katika Kijiji cha Kikagate, Kata ya Mubunda wilaya ya Muleba.

" Mradi wetu wa bomba la mafuta ulipaswa kumalizika rasmi Julai mwaka huu lakini kutokana na kuchelewa kwa vipuli ambavyo vinapatikana nje ya nchi vimekwamisha mradi huu utaanza rasmi Februari mwaka kesho kwa sasa uko asilimia 88"amesema Moshi.

Moshi amesema TPDC, inamiliki asilimia 15 ya hisa katika EACOP, imepata uzoefu mkubwa kupitia utekelezaji wa mradi huo, hususan katika ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi katika kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati.

Amesema, manufaa ya mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) yanaendelea kuonekana mkoani Kagera, huku ujenzi wa kituo cha kusukuma Mafuta Ghafi Namba Tatu (PS3) katika Wilaya ya Muleba ukifikia asilimia 88.

Kituo hicho kilichopo katika Kijiji cha Kikagate, Kata ya Mubunda wilaya ya Muleba, kinatarajiwa kukamilika Septemba mwaka huu, baada ya ujenzi wake kuanza Aprili 2024.



Mradi wa EACOP unamilikiwa na TotalEnergies kwa asilimia 62, TPDC asilimia 15, Uganda National Oil Company (UNOC) asilimia 15 na CNOOC Limited ya China asilimia 8.

Baadhi ya wakazi wa wilaya Muleba mkoani Kagera wamesema kuwa, mradi wa bomba la mafuta ukikamilika utachochea shughulu za kiuchumi katika maeneo unapopita mradi huo.

Mmoja wa wananchi wilaya ya Muleba Selestina Byamungu amesema, kuna wakazi wa wilaya hiyo walishanufaika kwa kujengewa nyumba pamoja na kupata fidia mradi huo unapopita.

Amesema mradi huo ukikamili anatatajia uchumi wa wananchi utaongezeka.



No comments