HEADER AD

HEADER AD

SERIKALI YARIDHIA WAFANYABIASHARA WAENDELEE KUUZA WANYAMAPORI WADOGOWADOGO


Na Alodia Dominick, Ngara

SERIKALI hapa nchini imeridhia wafanyabiashara waliokuwa wanafanya biashara ya kuuza wanyamapori hai wadogo wadogo kama nyani kuendelea kufanya biashara hiyo.

Hayo yamesemwa na Waziri wa maliasili na utalii dkt. Ashatu Kijaji akiwa katika mradi wa maji kijiji cha Rusumo wilaya ya Ngara wakati wananchi walipokuwa wanatoa kero zao kwa kiongozi huyo na kueleza kero za wanyamapori zinazowakumba katika maeneo yao.

Dkt. Kijaji amesema, serikali imeridhia watanzania kufanya biashara ya wanyama wadogo kama nyani kwani jambo hilo litapunguza wanyama hao kusumbua wananchi.

  Waziri wa maliasili na utalii dkt Ashatu Kijaji akipokelewa wilaya ya Ngara.

"Rais Samia ameridhia rasmi watanzania waliokuwa wanafanya biashara ya wanyama pori hai wakiwemo nyani au wanyama wadogo wadogo kama nyani na vipepeo, hatuuzi simba, hatuuzi tembo" amesema Dkt. Kijaji

Amewataka wafanyabishara ya Rusumo kuchangamkia fursa hiyo ili waweze kupunguza wanyama hao wanaokwenda hadi kwenye nyumba za wananchi.

Awali,mmoja wa wananchi katika kijiji cha Rusumo Jaredi Joseph amesema kuwa, yupo mtoto kijijini humo aliyeshambuliwa na nyani na kujeruhiwa na kusababisha mtoto huyo kupelekwa hospitali lakini ofisi ya maliasili na utalii haikutoa fidia yoyote kwa familia hiyo wakati aliyejeruhi ni mali yao.

        Jeradii Joseph mkazi wa kijiji Rusumo akitoa kero ya wanyamapori inayowakabili wananchi.

"Nyani na tembo wanaleta changamoto kubwa kwa wananchi kuna nyani alingata mtoto wa mtu mtoto huyu akapelekwa hospitali, lakini haukuwepo msaada  kwa mzazi huyo kutoka maliasili na utalii" amesema Jaredi

Ametaja changamoto nyingine ya kushambuliwa na tembo jambo linalopelekea uharibifu wa mazao mashambani.

Kamishna msaidizi wa hifadhi ya Burigi Chato Hokoro Mngofi ameeleza kuwa, wataandaa mafunzo ambayo yatasadia kuwajengea uwezo wananchi jinsi ya kujihami na wanyama pori na kutoa taarifa pindi wanapoonekana kwenye mazingira.

     Kamishna msaidizi hifadhi ya Burigi chato Hongoro Mngofi akitoa ufafanuzi juu ya wanyama  pori wanaoshambulia wananchi.

No comments