MWANDISHI WA HABARI DAUD JULIUS ALIYEKAMATWA APATA DHAMANA
Anaandika Edwin Soko
MWANDISHI wa habari Daud Julius maarufu King Davy wa Tarime TV, toka Tarime, Mkoa wa Mara ambaye nilitoa taarifa ya kukamatwa kwake Tarime na kusafirishwa kuja Mwanza, usiku huu baada ya kufikishwa Mwanza amepata dhamana.
Usiku huu nimefanya mazungumzo na RCO wa Mwanza na ambaye alitoa maelekezo kama kuna mtu wa kumdhamini aweze kumdhamini .
Nimefanikiwa kumtuma mwanachama wetu wa MPC na MISA Tanzania Maganga Gwesega kwa ajili ya kumdhamini mwenzetu na tumefanikiwa amepata dhamana mida ya saa tatu usiku.
Tuhuma za kosa ni matumizi mabaya ya mitandao kwa kusambaza clip ya video ya maamuzi ya kesi ya mahakamani, hivyo atarudi kesho Agosti 10, 2026 kuripoti.
Binafsi namshukuru sana RCO Mwanza kwa ushirikiano wake, Pia Maganga Gwesaga.
Tunawashukuru wote kwa ushirikiano wenu.
Mwenyekiti wa chama cha Waandishi wa habari mkoa wa Mwanza, Edwin Soko.Mwandishi wa Habari Daud Julius akamatwa na Jeshi la Polisi
Nimepokea taarifa ya kukamatwa kwa Mwandishi wa Habari Daud Julius (Tarime TV), na Jeshi la Polisi Tarime, Mkoa wa Mara mchana wa leo Jumapili, Agosti 9, 2026
Nimeongea na Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa kiwezesha waandishi wa habari Tarime, Helena Magabe amethibitisha kukamatwa kwa mwandishi huyo.
Baada ya kukamatwa David Julius na Polisi walianza safari ya kusafirishwa na Polisi kuelekea Mkoa wa Mwanza.
Sababu za kukamatwa kwake na Jeshi la Polisi haijawekwa wazi hadi sasa.
Kwa sasa tunaendelea kufuatilia kujua sababu za kukamatwa kwake, hivyo tuendelee kuwa na subira wakati tunafuatilia.
Tunaliomba Jeshi la polisi liweke wazi sababu za kukamatwa kwake.
Imetolewa na Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Mwanza, Edwin Soko.


Post a Comment