KARIBUNI AL-WAFAA ENGLISH MEDIUM ISLAMIC PRIMARY SCHOOL NA AL- WAFAA ISLAMIC SEKONDARY SCHOOL_....

Singida imeshamiri, kwa shule nyingi hakika
Zinatamba kwa uzuri, vizuri zinasikika,
Zinayo mengi mazuri, ninawatoa mashaka,
Lakini Al- Wafaa ni shule bora zaidi
Al- Wafaa yasifika, kwa mazingira mazuri,
Yanavutia hakika, nayasema siyo siri,
Maua yamepambika, yananukia vizuri,
Lakini Al- Wafaa ni shule bora zaidi
Mabweni yakuvutia, watoto wafurahia,
Kwa ndani yanavutia, hata na kwa nje pia,
Nidhamu yazingatia, maadili na tabia,
Lakini Al-Wafaa ni shule bora zaidi
Za sayansi maabara, shule inajivunia,
Hakika zina ubora, kwa viwango zavutia,
Vifaa vyake imara, na tena vinavutia,
Lakini Al-Wafaa ni shule bora zaidi
Watoto inawalea, kwa dini kuzingatia,
Kiimani wanakua, tena kwa njema tabia,
Watoto inapokea, kwa sifa kuzingatia,
Lakini Al-Wafaa ni shule bora zaidi
Elimu mbili hutoa, ya mazingira na dini,
Vigezo huzingatia, vya kutoka wizarani,
Shule inajivunia, elimu yenye thamani,
Lakini Al- Wafaa ni shule bora zaidi
Ina walimu mahiri, tena waliobobea,
Wanafundisha vizuri, kwa vitabu kurejea,
Kwa kufundisha hodari, kila mbinu hutumia,
Lakini Al-Wafaa ni shule bora zaidi
Ni shule yenye thamani, kwa elimu kuthamini,
Inasifika nchini, kwa kushinda mitihani,
Inashinda mitihani, ya kitaifa na ndani,
Lakini Al-Wafaa ni shule bora zaidi
Namaliza kuandika, yale nilokusudia,
Mengi nimeyaandika, kwa shairi kupitia,
Shule imethibitika, kwa elimu kuitoa,
Lakini Al-Wafaa ni shule bora zaidi
Mtunzi Sirdody Dody
0724917212
_Kilimanjaro_
Post a Comment