MEYA KIBAHA AANZISHA KAMPENI YA KUWASHIRIKISHA WADAU KUTATUA CHANGAMOTO ZA KIELIMU
Na Gustaphu Haule , Pwani
MSTAHIKI Meya wa Manispaa ya Kibaha Dr.Mawazo Nicas ameanzisha kampeni maalum ya kuwashirikisha wadau wa maendeleo hususani wa viwanda juu ya kukabiliana na changamoto za kielimu katika shule mbalimbali zilizopo ndani ya Manispaa hiyo.
Kwa sasa kampeni ya Dr.Nicas imeanza kuhusisha Shule ya Msingi Lulanzi iliyopo Kata ya Picha ya Ndege inayohitaji bati na Shule ya Sekondari Mwambisi iliyopo Kata ya Kongowe inayohitaji mabweni ya kulala wanafunzi.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kibaha Dr.Mawazo Nicas.Dr.Nicas amekuwa akiendesha kampeni hiyo katika ziara yake aliyoianza Oktoba 07,2026 katika kiwanda cha Sabuni na Pampasi( KEDS ) kilichopo Kata ya Picha ya Ndege, kiwanda cha U-Fresh kilichopo Kata ya Kongowe na kiwanda cha Qounqurer kinachotengeneza Tishu kilichopo Mtaa wa MiembeSaba Kata ya Kongowe.
Akiwa katika kiwanda cha KEDS alipokwenda kukagua miundombinu ya kutolea maji kutoka kiwandani alikutana na uongozi wa kiwanda hicho na kisha kufanya kikao cha pamoja ambapo aliomba uongozi wa kiwanda hicho kusaidia bati za kupaua shule ya Msingi Lulanzi.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kibaha Dr.Mawazo Nicas akikagua mitambo ya kutengenezea tishu katika kiwanda cha Qounqurer Investment kilichopo Mtaa wa MiembeSaba Saba Kata ya Kongowe.Dr.Nicas amesema Shule ya Msingi Lulanzi kwasasa miundombinu yake sio salama kwa wanafunzi na walimu wao kwakuwa wakati wa mvua paa linavuja kutokana na bati zake kutoboka.
Amesema kipindi hiki chakuelekea katika mvua za El-nino hali inaweza kuwa mbaya zaidi kama hatua ya haraka haitachukuliwa hivyo ni lazima wadau hususani wa viwanda washirikishwe ili kuweza kuchangia ukarabati wa shule hiyo.
Dr.Nicas aliuomba uongozi wa kiwanda hicho kusaidia katika kuchangia bati za kupaua Shule hiyo ambapo amesema kama watachangia bati hizo watakuwa wamesaidia jamii kubwa ya Manispaa ya Kibaha.
Meya wa Manispaa ya Kibaha Dr.Mawazo Nicas akiwa katika kikao cha pamoja na uongozi wa kiwanda cha juisi cha U-Fresh Fresh kilichopo Kata ya Kongowe."Shule yetu ya Msingi Lulanzi inakabiliwa na changamoto ya paa kuvuja wakati wa mvua na nyinyi KEDS ni kiwanda kikubwa hivyo naamini mnaweza kutusaidia katika kurudisha kwa jamii kwa kupaua shule yetu,"amesema Dr.Nicas.
Dr.Nicas ameendelea na kampeni hiyo katika kiwanda cha kutengeneza juisi cha U-Fresh kilichopo Mtaa wa MiembeSaba Kata ya Kongowe mahali ambapo aliomba uongozi wa kiwanda hicho kusaidia bati 500 kwa ajili ya ujenzi wa mabweni katika Shule ya Sekondari Mwambisi iliyopo Kata ya Kongowe.
Akiwa katika kikao na uongozi wa kiwanda hicho Dr.Nicas amesema Shule ya Sekondari Mwambisi inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa mabweni hali ambayo inasababisha wanafunzi kutembea umbali mrefu jambo ambalo linapelekea wanafunzi kuwa katika mazingira magumu.
"Kiwanda cha U-Fresh ni kikubwa na sisi katika Manispaa yetu kuna shule ya Sekondari Mwambisi inahitaji bweni kwahiyo tusaidieni kupata bati 500 kwa ajili ya ujenzi wa bweni hilo,"amesema Dr.Nicas.
Katika kiwanda cha kutengeneza Tishu cha Qounqurer Investments Company Ltd kilichopo Mtaa wa MiembeSaba Kata ya Kongowe Dr.Nicas ameomba mifuko ya sarufi kwa ajili ya ujenzi wa bweni hilo na kufanikiwa kupata mifuko 100 ya saruji.
Meneja biashara wa kiwanda cha KEDS Derick Deodatus amesema kuwa wapo tayari kushirikiana na Serikali kupitia Manispaa ya Kibaha katika kuchangia shughuli mbalimbali za maendeleo.
Deodatus amesema kuwa ombi la mstahiki Meya wa Manispaa ya Kibaha limekubaliwa na litafanyiwa kazi huku aliomba uongozi wa shule na Kata waandae barua maalum juu ya ombi hilo ili waweze kulifanyiakazi.
"kiwanda chetu kimekuwa kikichangia jamii mara kwa mara na hata sasa tulikuwa tumeandaa msaada wa vyakula kwa ajili ya kusaidia jamii katika kipindi cha El-nino lakini na hili la kupaua shule ya msingi Lulanzi tumelichukua na kulifanyiakazi,"amesema Deodatus.
Nae afisa masoko na mahusiano wa kiwanda cha Qounqurer Investments Company Ltd kinachojihusisha na utengenezaji wa Tishu Robert Baclay amesema kiwanda chake kitachangia mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa bweni la shule ya Sekondari Mwambisi.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kibaha Dr.Mawazo Nicas (kushoto) akizungumza na afisa Masoko na Uhusiano wa kiwanda cha Qounqurer Investments Company Ltd Robert Baclay(kulia).Baclay, amesema kuwa hatua ya uchangiaji huo ni muhitikio wa ombi la Meya wa Manispaa ya Kibaha lakini pia ni sehemu ya kusaidia jamii katika kuboresha mazingira ya elimu kwa wanafunzi ili waweze kufanya vizuri katika masomo yao.
Hata hivyo, amesema ataendelea kushirikiana na Serikali katika kutatua changamoto mbalimbali katika elimu, afya na hata katika sekta nyingine muhimu pale inapobidi.






Post a Comment