WAJUMBE WA BODI YA USULUHISHI KATA YA MSATA WARIDHISHWA NA ELIMU INAYOTOLEWA NA WATAALAMU WA KAMPENI YA MSAADA YA MAMA SAMIA
Na Gustaphu Haule, Chalinze
WAJUMBE wa bodi ya usuluhishi wa migogoro ya ndoa katika Kata ya Msata Halmashauri ya Chalinze Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani wameridhishwa na mafunzo yanayotolewa na wataalamu wa kampeni ya Msaada wa Kisheria wa Mama Samia kwakusema elimu waliyopata imewatoa matongotongo.
Kauli ya wajumbe hao imekuja mara baada ya kumalizika kwa mafunzo ya kuwajengea uwezo yaliyofanyika Novemba 4,2026 katika ofisi ya Mtendaji Kata ya Msata kupitia wataalamu wa msaada wa kisheria wa Mama Samia ( Mama Samia Legal Aid Campaign).
Wajumbe wa bodi ya usuluhishi wa migogoro ya ndoa Kata ya Msata Halmashauri ya Chalinze wakimsikiliza kwa makini mwezeshaji wa mafunzo ya kuwajengea uwezo ya msaada wa kisheria ya Mama Samia Marwa Mohere ( hayupo pichani).Mafunzo hayo yalikuwa yakitolewa na mratibu wa Kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia ambaye ni wakili wa Serikali kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Marwa Mohere akisaidiana na mwanasheria wa Halmashauri ya Chalinze Elizabeth Lukumay.
Katibu wa bodi ya usuluhishi wa migogoro ya ndoa Kata ya Msata Hamisi Issa, amesema kuwa wameyapokea mafunzo hayo kwa mikono miwili kwakuwa mambo mengi waliyofundishwa walikuwa hawayajui.
Issa amesema kuwa mafunzo hayo yamekuwa na mambo mengi mapya na wameyajua katika kampeni hiyo na kwamba bila kufanyika kwa kampeni hiyo wasingepata uelewa kama ambavyo wamepata hivi sasa.
Mratibu wa Kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia katika Halmashauri ya Chalinze ambaye ni wakili wa Serikali kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Marwa Mohere (katikati)mwenye T shirt nyekundu) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi ya usuluhishi wa migogoro ya ndoa wa Kata ya Msata .Ameongeza kwasasa wamejua kuwa wanapokaa na kusuluhisha migogoro ya ndoa wanaitwa wajumbe wa bodi ya usuluhishi lakini wanapokaa na kusuluhisha migogoro ya ardhi jina linabadilika na kuwa baraza la Kata .
Amesema pamoja na hilo, lakini wametambua kuwa bodi ya usuluhishi wa migogoro ya ndoa inanguvu na mamlaka makubwa ya kusaidia jamii na hivyo kufikia haki zao kwa mujibu wa sheria.
"Tumeyapokea mafunzo haya kwa mikono miwili na tutaendelea kuyatumia katika usuluhishi wa migogoro ya ndoa kwa kufuata miongozo tuliyofundishwa kwakuwa sasa hivi tumepata elimu ambayo sote hatukuwanayo na tulikuwa tunafanyakazi kwa mazoea tu,"amesema Issa.
Nae Shukuru Pesa,amesema kuwa anampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutambua umuhimu wa bodi za usuluhishi wa migogoro ya ndoa na mabaraza ya Kata kwa kuwapa elimu na kuwajengea uwezo.
Mmoja wa wajumbe wa bodi ya usuluhishi wa migogoro ya ndoa katika Kata ya Msata ( kushoto) akizungumza na mratibu wa Kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia Marwa Mohere mara ya baada ya kuwajengea uwezo katika mafunzo yaliyofanyika Novemba 4,2026 ofisi ya Kata Msata.Pesa,amesema amefurahi kuona hata wao wanafikiwa kwa kupewa elimu na kwamba kwa miaka mingi iliyopita hawakuona uongozi ambao unawajali na kuwafikia kama Serikali ya awamu ya sita.
"Naomba nipelekeeni salamu zangu kwa Rais Samia kwani kitendo alichokifanya ni kututoa matongotongo na kutupa mwanga wa kufahamu ni kitu gani wajumbe wa bodi wanapaswa kufanya lakini hata uelewa tuliopata ni mkubwa na utakwenda kutumika kusaidia wananchi wa Kata ya Msata na jamii kwa ujumla ,"amesema Pesa.
Mratibu wa Kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia ( Mama Samia Legal Aid Campaign) ambaye ni wakili wa Serikali kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Marwa Mohere amesema kuwa bodi hizo zimeundwa kupitia kifungu cha 103,sura ya 29 ya sheria ya ndoa ya mwaka 2023.
Mratibu wa Kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia katika Halmashauri ya Chalinze Marwa Mohere akitoa mafunzo ya kuwajengea uwezo wajumbe wa bodi ya usuluhishi wa migogoro ya ndoa wa Kata ya Msata, Novemba 04,2026.Mohere,amesema kuwa wajibu wa bodi hizo ni kufanya usuluhishi na sio kutoa hukumu wala maamuzi yoyote lakini pia ina Mamlaka ya kusikiliza pingamizi ya ndoa na kutoa mapendekezo pamoja na kutunza kumbukumbu za ndoa.
Hatahivyo, Mwanasheria wa Halmashauri ya Chalinze Elizabeth Lukumay amewataka wajumbe wa bodi ya usuluhishi wa migogoro ya ndoa kuacha kutumia lugha ya ubabe katika kusikiliza malalamiko na badala yake watumie lugha ya upole na heshima.
Lukumay,amesema kuwa kama watatumia ubabe matokeo yake yule ambaye analeta malalamiko atakuwa anashindwa kueleza shida yake na hivyo kupoteza imani na bodi hiyo.
Katibu wa bodi ya usuluhishi wa migogoro ya ndoa Kata ya Msata Hamisi Issa (kushoto) akisikiliza maelekezo kutoka kwa Mwanasheria wa Halmashauri ya Chalinze Elizabeth Lukumay katika mafunzo ya kuwajengea uwezo yaliyofanyika Novemba 04,2026 katika ofisi ya Mtendaji Kata ya Msata Halmashauri ya Chalinze Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani.





Post a Comment