HEADER AD

HEADER AD

WAZIRI ULEGA AIPONGEZA TAKUKURU PWANI KWA KUJITAHIDI KUZUIA RUSHWA NA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI


 Na Gustaphu Haule, Pwani

WAZIRI wa Katiba na Sheria Abdallah Ulega ameipongeza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa  (TAKUKURU) mkoa wa Pwani kwa kuendelea kutekeleza wajibu wake wa kuzuia rushwa na kutoa elimu kwa wananchi.

Ulega ametoa wito huo Novemba 28/2026 wakati alipotembelea banda la TAKUKURU katika ufunguzi wa kampeni ya msaada wa Kisheria ya Mama Samia awamu ya pili uliofanyika katika viwanja vya stendi ya zamani Mailimoja katika Manispaa ya Kibaha.

       Waziri wa Katiba na Sheria Abdallah Ulega (wa pili kulia) akitembelea banda la Takukuru Mkoa wa Pwani ikiwa ni sehemu ya ufunguzi wa Kampeni ya msaada wa Kisheria ya Mama Samia.

Amesema TAKUKURU imekuwa ikifanyakazi kubwa katika kuzuia na kupambana na rushwa lakini hata jitihada za kutoa elimu kwa wananchi zinaonekana kupitia vyombo mbalimbali vya habari.

Ulega amewaomba wananchi kuhakikisha wanaendelea kushirikiana na Takukuru kufanikisha malengo yake kwakuwa wanachokifanya ni kusaidia katika kusukuma gurudumu la Maendeleo hapa nchini.

        Wananchi wa Mkoa wa Pwani wakishiriki ufunguzi wa Kampeni ya msaada wa Kisheria ya mama Samia awamu ya pili katika viwanja vya stendi ya zamani Mailimoja.

"Kwa kweli TAKUKURU inafanyakazi kubwa na Serikali inatambua umuhimu wake na sisi kama Wizara ya Katiba na Sheria tupo tayari kuendelea kushirikiana ili tuweze kuifikisha nchi katika hatua ya juu ya Maendeleo,"amesema Ulega.

Ulega ameongeza kuwa wanapofungua kampeni ya msaada wa Kisheria ya Mama Samia ni wazi kuwa TAKUKURU wanahusika moja kwa moja kwakuwa ndio majukwaa ambayo wanaweza kuyatumia kwa kutoa elimu kwa wananchi.

Mkuu wa dawati la uelimishaji TAKUKURU mkoa wa Pwani Aneth Mwakatobe, amesema kuwa wametumia ufunguzi wa kampeni ya msaada wa Kisheria ya Mama Samia kwa kutoa elimu kwa wananchi.

        Mkuu wa Mkoa wa Pwani Stanslaus Nyongo akizungumza katika ufunguzi wa Kampeni ya msaada wa Kisheria ya mama Samia awamu ya pili Oktoba 28/2026.

Mwakatobe, amesema kuwa wanatoa elimu kwa wananchi wa Mkoa wa Pwani ili kuelewa faida na maana ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa na kwamba kutokana mapambano hayo wanaona faida za moja kwa moja.

"Tupo katika kampeni hizi za msaada wa Kisheria wa Mama Samia kwa ajili ya kutoa elimu itakayosaidia kuzuia rushwa kwahiyo niwaombe wananchi kuendelea kushirikiana kwa ajili kuhakikisha rushwa inatokomezwa," amesema Mwakatobe .

Mwakatobe ametoa wito kwa wananchi kufika katika ofisi za TAKUKURU zilizopo karibu na jengo la benki ya NMB katika Manispaa ya Kibaha kwa ajili ya kutoa taarifa za rushwa au kwa kupiga namba ya simu bure 113 .

Hatahivyo, Mwakatobe amewashauri na kuwaelekeza wananchi kuacha kujihusisha na vitendo vya rushwa na kwa yeyote ambaye atabaini vitendo hivyo atoe taarifa TAKUKURU.

     
Waziri wa Katiba na Sheria Abdallah Ulega akiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali katika ufunguzi wa Kampeni ya msaada wa Kisheria ya mama Samia awamu ya pili kwa Mkoa wa Pwani.

No comments